Paroles de Niombee
Paroles de Niombee Par MOTRA THE FUTURE
Niombee
Usiku mchana Niombee
Kila siku Niombee
We Niombee
Nakuomba Mama Yangu Niombee
We Niombee
Niombee
Usijali soon mama nitakuja Nakuomba Niombee
Usichoke Niombee
We Niombee
Ooouuyeeh
Hello mama, shkamoo mama
I hope hapo home mumeamka salama
Mi bado niko bongo pande ya daresalama
Tunaparangana ila nawakumbuka banana
Leo nimepiga simu nikuhadithie ka story
Jinsi gani huku mambo ilikuwa ni ngori
Ukiona kimya sometimes wala usiworry
Si unajua maishani ushindi ni kugombania goli
Nshakaa sikutatu hata kubonya sijabonya
Sikuwa na pa kukaa wala pa kupata moranya
Enzi hiyo niko lebo hapo Kinondoni kwa mona
Kabla ya Samaki kujikuta tumboni kwa yona
Sikuhizi sikai gheto na machalii ninapanga
Saa hii sikai kino saa hii ninakaa changa
Maisha imechange now kidogo hata ninapanda
Ni siku nyingi sana daladala sijapanda
Najuana na watu kidogo wananisevu
Ila huu u braza braza unaweza ukakufanya slave sometimes
Usipakuwa na akili yako
Unaweza hata ukshtakiwa na wakili wako
Niombee
We niombee
Usijali mama angu niombee nitakuja niombee
We niombee
Huku mjini mambo mengi kila siku hupambana niombee
We niombee
Usijali vitu vyema vinakuja nakusihi niombee
We niombee
Niombee usichoke niombee
Kila muda niombee
Nishapitia mengi na mengine ni aibu
Shkuru tu Mwanao sijapitia uraibu
Kitu cha mtu sijawahi kuharibu
Kurudisha ukaribu
Bado na braza masebo najaribu
Nakuskia hapo unakimbizana na kuku
Wamefika wangapi saa hii si kama buku
Usiskize story za mitandao maana huku
Category za Rap tunashindana na zuchu
Mwali wako yuko nje anasukana mabutu
Ngoji nimtume kwa wakala akutumie ka luku
Usijali leo naanza kukupunguzia machungu
Halafu kesho nikutumie za nyama ya nundu
Unakumbuka ule muda nlikwambia mambo inasonga
Ilikuwa haisongi nilikuwa tu ninabonga
Sikutaka kukukatisha tamaa ya kuniombea
Kuna time nakwambia nlitamani hata kujinyonga
Ilaaa nikakazana kukicha ili kubanmba
Nishafeligi kitu sijafanya ni kusanda
Hata pale nliporudi kukaa ghetto kwa mdogo o
Wangu wa kike na tukashea moja kitanda
Sijawashi gusa tungi wala sijawahi gusa ganja
Na ningeacha maombi
Ingekuwa saa hii ni Matanga
Tena vile wanga Ndo wameshikana na Anga
Ntakuja nikuhadithie
Story ya mi na dogo janja
Niombee
We niombee
Usijali mama angu niombee nitakuja niombee
We niombee
Huku mjini mambo mengi kila siku hupambana niombee
We niombee
Usijali vitu vyema vinakuja nakusihi niombee
We niombee
Niombee usichoke niombee
Kila muda niombee
Niombee
Mmmmmh
Eeeeeeeee
Iiiiiye iyeee
Mama We niombee tuu soon tunashinda
Mishale mingi ila maombi yako ni kinga
We niombee tu
Ecouter
A Propos de "Niombee"
Plus de Lyrics de MOTRA THE FUTURE
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl