IBRAAH Bado ( Magufuli )  cover image

Paroles de Bado ( Magufuli )

Paroles de Bado ( Magufuli ) Par IBRAAH


Siamini ndoto zimeishia njiani
Baba shupavu we huko tena duniani
Na ulituahidi utafikisha taifa
Pale pale baba Magu

Nyuso ya taifa imetawala huzuni
Kukurudisha ndo hatuwezi jamani
Na kazi ya Mungu huwezi pinga abadani
Ayee ayee baba Magu

Baba umeondoka taifa umemuachia mama
Na hatuna cha kufanya tunalia wana
Wote twasema bye bye
Twasema bye bye, hatuna budi

Baba umeondoka taifa umemuachia mama
Na hatuna cha kufanya tunalia wana
Wote twasema bye bye
Twasema bye bye, hatuna budi

Nikitazama taifa ulivyojenga hata siamini
Eti Magu umeondoka kweli haingii akilini
Ha roho inaniuma mimi baba, baba
Baba Kikwete analia hadi na Baba mwinyi
Na Kassim Majaliwa bado hatuamini
Kama umetutoka baba baba

Ila baba, bado, bado
Bado hatuamini bado, bado, bado
Kama kweli we umetangulia, bado
Oh kuamini bado inakuwa ngumu, bado bado
Bado, bado bado, bado hatuamini bado

Maneno yako yatakumbukwa daima we baba shupavu
Ulizo amini wajane hadi walemavu
Magufuli we ulijaa wema
Ulikuwa ni mwingi wa huruma

Haya sawa tuishi bila matabaka, ni wewe
Elimu bure kusoma bila mipaka, ni wewe
Ulideal na wala rushwa waiba sadaka, ni wewe
Ni wewe na ni wewe

Na wamachenga tufanye kazi popote, ni wewe 
Ulisimama baba we ulitutetea
Leo twatokwa machozi twakulilia 
Ni wewe ni wewe

Bado, bado baba, bado, bado
Bado hatuamini bado, bado, bado
Kama kweli we umetangulia, bado
Oh kuamini bado inakuwa ngumu, bado bado
Oh bado hatuamini bado

Ecouter

A Propos de "Bado ( Magufuli ) "

Album : Bado ( Magufuli ) (Single)
Année de Sortie : 2021
Copyright : (c) 2021 Konde Music
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Mar 20 , 2021

Plus de Lyrics de IBRAAH

IBRAAH
IBRAAH
IBRAAH
Leo
IBRAAH

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl