BANDO Captain  cover image

Paroles de Captain

Paroles de Captain Par BANDO


Ambia mitaa
Shytown boy
Ambia mitaa
Ambia mitaa situmefika
Tukichafua pilika pilika

Maongezi baada ya kazi badae kaka tuchat
Ngoma ya uswahili itambae mpaka masaki
Ukiskia ubao ijia chaki
Maana bongo hupati haki hata ukitangulia mbele za haki
Ndo yalivyo maisha ya binadam jau
Unaeza ukafa njaa siku ya msiba wako wakapika pilau
Weka mipaka isifike minyau
Maana kuna muda hata dr kumbuka anajisahau
Wananiita captain mzee wa anga
Shetani hawezi kumiliki nyumba hata kama mungu amepanga
Mapenzi ni ushamba
Dem wako unamlea kama yai kumbe kuna wahuni wanamkaanga
Tuliyopitia ndo yamejenga confidence
Maisha yenyewe hayataki hata hugompecate
Wakifunga milango tunavunja mageti
Wakiuliza nani waambie ni sisi eeh

Captain eeh
Captain mi ndo captain
Nahodha eeh
Nahodha mi ndo captain

Ambia mitaa
Ambia mitaa
Ambia mitaa situmefika
Tukichafua pilika pilika

Haya usiniletee mipango kama huna hata mia
Usinishikie mabango wee usinizibie njia
Chuki ndo kitu ambacho nachukia (nachukia)
Na ujinga namba moja nikuuza mlango ili ununue pazia
Na usile usichokilisha utaliwa
Endeleenu kubisha
Imeandikwa kila atakae bisha atafunguliwa
Namba ni pure chafu kabisa imekataliwa
Alafu hatucheki na watoto wasije kutuomba maziwa
Unaambiwa gundi huwezi gundisha kwa gundi
Ukinona mama wa kambo anakupenda ujue baba ako fundi
Wape habari chombo naiendesha mimi
Kikojozi hapati usingizi ugenini
Wananiita captain mzee wa anga
Shetani hawezi kumiliki nyumba hata kama mungu amepanga
Mapenzi ni ushamba
Dem wako unamlea kama yai kumbe kuna wahuni wanamkaanga
Tuliyopitia ndo yamejenga confidence
Maisha yenyewe hayataki hata hugompecate
Wakifunga milango tunavunja mageti
Wakiuliza nani waambie ni sisi eeh

Captain eeh
Captain mi ndo captain
Nahodha eeh
Nahodha mi ndo captain

Ambia mitaa
Ambia mitaa
Ambia mitaa situmefika
Tukichafua pilika pilika

Ecouter

A Propos de "Captain "

Album : Captain (Single)
Année de Sortie : 2023
Ajouté par : Farida
Published : Aug 04 , 2023

Plus de Lyrics de BANDO

BANDO
BANDO

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl