FID Q Bendera Ya chuma cover image

Bendera Ya chuma Lyrics

Bendera Ya chuma Lyrics by FID Q


Naitwa Farid kwa maana mi ni wa pekee 
Na wa aina yake
Huu ujasiri na utajiri wa mashairi wa tafsiri zake
Jasiri ka usiogope kuumia
ukiwa na noti utumia
Kina kinduta, kina pochi wakazia
Tajiri wa mashairi mi sio hodari wa kurap tu
Mi sio msanii nafanya hii kwa ajili ya watu
Nina uso wa mbuzi na ninapewa front page
Na daily kwenye news sina skendo yoyote

(wapi, wa.wapi)
Wapi niliwakosea?
Wapi mie siku-play fair?
Sikuzaliwa niwe kamili, nilizaliwa niwe real yeah
Na udhaifu hauna dili, kwani strong naji-feel here
Nadhifu kiakili, street smart, brush and spear
Nipo ili nife maisha sio mchezo wa uoga, mjomba
Unataka nshibe hakikisha haukombi mboga, bomba
Nipake tope nijikombe kombe mafuta
Uniponde unizonge kutwa
Nikonde mnyonge wa kutupwa
Kwa mgongo wa chupa nipake nisijepauka
Ntaibuka tu kama vumbi dongo likija kukauka

Mi nateleza, nakosea
Naanguka, napotea
Najifunza kuendelea
Nainuka natembea
Nateleza, nakosea
Naanguka, napotea
Najifunza kuendelea
Nainuka natembea
Bendela ya chuma, inapepea
Bendela ya chuma
Bendela ya chuma, inapepea
Bendela ya chuma

Nachunga hasira isiniumize ili maumivu yasintishe
Hawaishi hila wenye wivu, wanazingira nisipite
Dua haziishii angani, ua linazaa bustani
Bahati haina ahadi, ikihitaji hutua ndani
Sihofii kudondoka sababu mi 'na mabawa
Wanaofikiria ntachoka, wanaogopa Ngosha ana power
Cheusi ni mzawa, Cheusi hana dawa ya kutoka
Pagawa ukitosa, kosa kunawa kabla haijatosha
Kivipi uniache wakati mziki upo na mie?
Kwake nina mapenzi ya mswaki
Sitaki mwingine achangie
Masika bila mbu, sio gharika bila Nuhu
Shida nazo kila mtu, chakarika uje unafuu

Hekima ni kukosa excuse
Kukosa excuse unapo-lose
Na pia ukishinda usiji-boost 
Usiji-boo siamini makuuzi
Hekima ni kukosa excuse
Kukosa excuse unapo-lose

Mi nateleza, nakosea
Naanguka, napotea
Najifunza kuendelea
Nainuka natembea
Nateleza, nakosea
Naanguka, napotea
Najifunza kuendelea
Nainuka natembea
Bendela ya chuma, inapepea
Bendela ya chuma, inapepea
Bendela ya chuma, inapepea
Bendela ya chuma

Nafanya nakaa kama yule MC wa Kenya
Ukisikia pah jua haikupangwa ufe mapema
Sikuiti shujaa kwa kufanye kile unachofanya
Ntakuita mjinga ukiwa ukishindwa wakati
chawezekana
Dunia ni kubwa pia ni ndogo ka tukiungana
Ki utu uzima
Na mlima haupandwi kwa kuutazama
Ningekuwa kisiwa maisha yangekuwa ufukweni
Huu upeo nimetunukiwa na Mungu wangu basi nipokeeni
Inatosha? Wanasema hapana, dondosha
Na tena wanaochana hawajiiti conscious
Ni Ngoshious!


About Bendera Ya chuma

Album : Bendera Ya chuma (Single)
Release Year : 2019
Added By : Afrika Lyrics
Published : Aug 25 , 2019

More FID Q Lyrics

FID Q
FID Q
FID Q

Comments ( 0 )

No Comment yet


Kelxfy

About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2022, We Tell Africa Group Sarl