Napungukiwa Nini Lyrics
Napungukiwa Nini Lyrics by JAPHET ZABRON
Ndege, hawavuni
Hawapandi wala hawafanyi kitu
Mihangaiko, ya dunia sahau wala hawasumbukii
Sauti tulivu
Asabuhi huimba nakushukuru
Wanamjua awapae kuishi kamwe hawahofu kitu
Heeh’ ndivyo aishivyo amtumainie, muumba wa mbingu
Hahangaiki hahofii dunia na masumbuko yajayo
Napungukiwa nini, Napungukiwa nini
Nikiwa naye Yesu
Sina kiu ya kitu
Napungukiwa nini, Napungukiwa nini
Nikiwa naye Yesu
Sina kiu ya kitu
Huna tumaini
Umekwama na kesho inakutisha
Hufika muda
Peke yako, njiani waongea na kulia
Maisha mzigo
Umetengwa wapendwa kukukimbia
Nikukumbushe
Yupo Yesu rafiki hata usiwaze kitu
He he, ndivyo aishivyo
Amtumainie muumba wa mbingu
Hahangaikii hahofii dunia na masumbuko yajayo
Napungukiwa nini (nakosa nini)
Napungukiwa nini (zaidi nini Baba)
Nikiwa naye Yesu
Sina kiu ya kitu
Napungukiwa nini, Napungukiwa nini
Nikiwa naye Yesu
Sina kiu ya kitu
Mungu yupo upande wetu
Nani atakae kaa juu yetu
Tulia, tulia, tuliaa kwa Yesu
Watch Video
About Napungukiwa Nini
More JAPHET ZABRON Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl