Wimbo Wetu Lyrics by ETHAN MUZIKI


Sijawahi penda kupanda ndege
Hakuna kitu kitafanya nizoee
Ninahofia urefu sio siri
Ninatetemeka nikifiri
Lakini hii kazi nimechagua
Najua itabidi nitembee
Mara nyingi itaturusha
Pande tofauti za dunia ikifanyika
Simu nitachukua
Ili nisikize wimbo
Inirudishe kando yako na nitakupigia
Sauti nikisikia
Nitajihisi niko kwako, ukinihitaji hapo
Nitakukumbusha
Unaweza cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Ukinihitaji we’icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu
Huu ni wimbo wetu

Nakumbuka usiku juzi juzi
Umelala kando yangu mpenzi
Nafasi ni kubwa kitandani
Umechagua pande yangu lakini, na nikikuangalia
Jinsi umetulia
Nilijazwa na raha
Hii ni baraka, sana
Nikajipata
Karatasi nachukua
Nikuandikie wimbo
Nikuanikie roho
Ukiamka, afadhali utajua
Nakupa penzi dabo dabo
Ukinihitaji hapo nitakukumbusha
Unaweza cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Ukinihitaji we’icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu

Ukihitaji (Ukihitaji)
Nikuwe nawe
Wewe icheze, icheze
Cheza wimbo wetu
Ukinihitaji we’icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu
Huu ni wimbo wetu

Watch Video

About Wimbo Wetu

Album : Wimbo Wetu (Single)
Release Year : 2023
Added By : Farida
Published : Jul 07 , 2023

More ETHAN MUZIKI Lyrics

ETHAN MUZIKI
ETHAN MUZIKI
ETHAN MUZIKI

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl