Natubu Lyrics
Natubu Lyrics by CHIDI BEENZ
Mola nipende usije nichukia
Najua mi ni mzembe mengi napuuzia
Usiniache niende siko nzuri njia
Juhudi nije kwako goti kukupigia
Najua hunisahau bado upo nami
I believe that hata napokuwa njiani
Mengi unasafisha na kunitoa gizani
Huwa sipendi kukosea namshutumu shetani
Kipi nifanye ili nilinge
Nikudharau, nani mwingine anilinde?
Natubu sasa sitaki kuja sema ninge
Mi ni mja wako usinitupe unilinde
Maana mi nina issue, issue tu, issue tu
Miezi nane sijaswali lakini leo inabidi tu
Nani anaiongopea dira yake ipotee
Niwezeshe nimwone ili nimkembe
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi Baba
Mi sio tajiri sio low class
Nipo kati nitakacho naweza pata naweza kosa
Mwenye kuchacha dhawabu
Wingi wa makosa mi naamini
Sifa ndo sometimes zanipoteza
Nawaza siku ya mwisho, nina mengi ya kutubu
Nipunguzie mi japo nisije kuwa bubu
Niokoe niweze kukumbusha hata Ayubu
Mali yangu Paulo -- na ya bubu
Najua natembea ila zote nguvu zako
Najua naongea ila yote maneno yako
Napochanganya -- huwa shetani ananimix
Lakini - nguvu zako sitompa wa urahisi
Usiniache nipotee, mwovu niendelee
Mi si kitu mbele yako hata ndotoni unikemee
Nisipoteze dira nionyeshe njia mapema
Nisafishe niwe kama niliyezaliwa tena
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi Baba
Eeeh Mola dunia hii inakwisha
Tunauana kwa upumbavu na visa
Tamaa za madaraka kugombania nyadhifa
Swala kushangaa kuona damu inamwagika
Magonjwa yanazidi, maisha yanabana
Vifo vya mapema kwa watoto na vijana
Ndio kutusamehe umeshatusamehe sana
Na una zaidi ya hasira na hizi ni kama laana
Lakini bado tunataka rudi kwako sisi
Ingawa najua itakuwa sio rahisi
Tupunguzie japo haya mabalaa
Shetani katuzunguka ukimkimbiza anakataa
We ni zaidi ya yote muumba wa dunia
Wanadamu twendeni wote kumsujudia
Tumwombe atusamehe haya, asamehe madhambi yetu
Asitoke aendelee kuwa ndani ya mioyo yetu
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi Baba
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi
Aaah aki ya Mungu natubu
Na naacha hata mavurugu
Mi minapunguza visasi
Punguza maasi narudi kwako kwa kasi Baba
Watch Video
About Natubu
More CHIDI BEENZ Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl