BRIGHT Nimeyumba cover image

Nimeyumba Lyrics

Nimeyumba Lyrics by BRIGHT


Miaka tisa Dar, mambo yamefeli
Sina hata bajaji
Eti niuze mkaa ila sio kweli
Mbona sina mtaji

Nanga imepaa nawaza ukabaji
Ili nikidhi mahitaji
Yote yanakataa
Naogopa utapeli nitafungwa

Mara Bright siku hizi hatubambi
Toka amwagwe na management
Anachoimba sisi hatutaki
Anayoyafanya haeleweki

Aliniambia mama, mama 
Mwanaume kupambana nisichoke
Kuna mengi ya kufanya, fanya
Hata nikianguke niinuke

Tena alisema mama, mama 
Cha mtu sumu nisiguse
Kama imeshindikana, kana
Nirudi nyumbani nisilazimishe

Nimeyumba, nimeyumba
Nimeyumba, nimeyumba
Nimeyumba, nimeyumba

Wako wapi wale walosema
Kwamba ni shabiki wa damu
Tena walishika bango
Whatsapp wakaunga team

Redio hawapigi hata ngoma
Maisha yamekuwa magumu
Sina show mapromoter tena
Hawapigi hata simu

Au tayari ndo tayari
Nilowakuta warejee ndani
Stress zinilaze chali
Niwe kulewa dawa kali

Au tayari ndo tayari
Nilowakuta warejee ndani
Stress zinilaze chali
Niwe kulewa dawa kali

Aliniambia mama, mama 
Mwanaume kupambana nisichoke
Kuna mengi ya kufanya, fanya
Hata nikianguke niinuke

Tena alisema mama, mama 
Cha mtu sumu nisiguse
Kama imeshindikana, kana
Nirudi nyumbani nisilazimishe

Nimeyumba, nimeyumba
Nimeyumba, nimeyumba
Nimeyumba, nimeyumba

Amesahaulika Juma Nature
Yuko wapi Inspekta
Atakayeumiza nesi hamtaki kabisa
Ona PNC Tonya mbili
Malovi hambembelezi tena
Bwana misosi, MarTi
Afande tena simba hang'ati tena
Wameyumba

Chelea Mani, Dazi baba
Ferooz wa starehe, wameyumba
20 percenti yule Sparki simwoni pasha ee
Wameyumba

Kila kibanda cha simu Sogi dogi
King Prais ke
Wapi Stara Tomasi Sista P eeh
Wameyumba
Dume bwege kaka Bushoke 
Eeh ameyumba
Baraka the Prince

Watch Video

About Nimeyumba

Album : Nimeyumba (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 20 , 2021

More BRIGHT Lyrics

BRIGHT
BRIGHT
BRIGHT
BRIGHT

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl