Ndoto Lyrics by BEST NASO


Mji siujui jina lake
Mji siijui nchi yake 
Ni kwenye ndoto

Nimekutana naye John Pombe Magufuli
Jana kwenye ndoto (Kwenye ndoto)
Ilikuwa kwenye mji wa kifahari
Mji wenye vingi vyote vizuri

Ooh mara napita naskia nimeitwa
Tena na sauti ambayo naikumbuka
Nikamwona John Pombe nikahisi furaha
Ameketi pazuri pa kifahari, ooh John
Akanikaribisha na neno zuri la kuchekesha
Akauliza, akauliza vipi kuhusu Tanzania yangu
Unamwonaje mama Samia, ulivyoondoka mzee amezushwa mengi
Kama uijuavyo Bongo (Bongo)

Jakaya mzee Kinena walizushiwa wamekuua
Ni nani alisambaza upuzi huo
Kifo changu asihusishwe mtu yeyote
Mimi nilikuwa na maradhi yaliyokuwa yananisumbua
Kwa muda mrefu kidogo, na muda umefika Mungu amenichukua
Ukweli unabaki ukweli

Mzee Tanzania imekumiss, tena imemiss ile mikiki mikiki
Mzee ile siku ya kifo chako ulichanganya kifo sana
Afande Sele bila uoga akamtukana Mungu akakufuru
Kuna wengine waliokuja kukuaga uwanja wa Taifa wakafa (Johnny)
Wale wamama uliokuwa unawatetea walisikia matoki imeingia

Ndugu zangu nawapa pole sana
Na vipi kuhusu mama Samia anaeneza vizuri mikakati yangu
Ndivyo mama Samia tena anapendwa kweli kweli
Ila tatizo ni mpole sana mama

Na nimesikia baada ya kifo changu kuna watu wamenisaliti
Mzee ndivyo dunia tambara mbovu
Hata ufanye vipi ukasifiwa
Ukifa huwezi kosa msaliti

Huo ni ukweli kijana wangu
Tena ukweli wa Mungu
Na vipi kuhusu mama Janet Mke wangu 
Wanamtunza au?

Ooh mama Janet hali yake haielezeki
Ila ndio hivyo imebidi Mungu kakupenda hana budi
Unajua nilikuwa napenda sana kamziki
Vipi kuhusu Alikiba, Diamond na kijana wangu Harmonize

Mzee game imechangamka ingawa vibeef ndo zinaamka 
Sasa kwa nini usiwashauri vijana wenzako wabadilike
Waache mabeef 
Mzee watu wana vichwa ngumu yaani kama vile wanavuta bangi
Na kuhusu baba Levo na H Baba
Mzee utaniingiza kwenye ugomvi
Chonde chonde mzee hao siwawezi

Nimekuelewa sasa nakupa maaagizo upeleke
Mwambie mama Samia namwamini kweli kweli
Najua mama Samia ni chuma kweli kweli
Tumefanya naye kazi awamu ya tano
Sijaona tatizo lolote kwake
Na naamini atakwenda kufanya mambo mazuri
Ya kuwafurahisha waTanzania

Lakini jambo kubwa mwambie
Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni
Muda mwingine awe mkali
Mara eeh nikashtuka ndoto
(Moja Moja Records)

 

Watch Video

About Ndoto

Album : Ndoto (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jun 29 , 2021

More BEST NASO Lyrics

BEST NASO
BEST NASO
BEST NASO

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl