Mahabuba Lyrics by BEKA IBROZAMA

Beiby, nataka nikung'ate sikio 
Nilo nayo ndani
Beiby, nishalipata chungio
Nichengeze pumba za Pwani

Mvuvi haogopi chombo
Nipe nivue
Kagere hachezeshwi ndondo
Sijisumbue

Miuno ya paka chongo
Nisasambue
Penzi lizidi uhondo
Uhondoo

Mahaba! Zidisha mahaba nidate
Mahaba! Kwa joto baridi nikumbate
Mahaba! Uwe ulimi niwe mate
Mahaba! Mahabuba aaah...

Watakuja kwa hodi ngongongo
Kusudi waniibie, wengine vimacho zongo
Hodari wa kupiga madongo
Wasije kukupa hongo

Mwenzako nina moyo wa kizamani
Nikipenda napenda mazima
Mie joka wa kijani
Vurugu huwaga sina

Sa wasije wanyang'anyi 
Mizizi wakakata na shina
Mi nitabaki na nani?
Bila wewe...

Mvuvi haogopi chombo
Nipe nivue
Kagere hachezeshwi ndondo
Sijisumbue

Miuno ya paka chongo
Nisasambue
Penzi lizidi uhondo
Uhondoo..

Mahaba! Zidisha mahaba nidate
Mahaba! Kwa joto baridi nikumbate
Mahaba! Uwe ulimi niwe mate
Mahaba! Mahabuba aaah...

Mahabuba ooooh
Mahabuba aaah
Mahabuba
Mahabu---uuuh

Music Video
About this Song
Album : Mahabuba (Single),
Release Year : 2019
Copyright : (c) 2019
Added By: Huntyr Kelx
Published: Aug 09 , 2019
More Lyrics By BEKA IBROZAMA
Comments ( 0 )
No Comment yet