ASLAY Likizo cover image

Likizo Lyrics

Likizo Lyrics by ASLAY


Message zako nimeziona
Ati umechoka visa vyangu
Oooh mama

Mbona unakufuru Mungu
Si ungesema kama umechoka penzi langu
Oh mama

Nijitakatae, ale tate nane
Hutaki hata tuonane
Vibaya hivyo
Oh mama, oh tate nane
Unapenda tufokeane
Vibaya hivyo ooh mwana

Nakuonaga tu snapchat
Au Insta picha ukiposti
Ni block basi mama nisikuone
Anakujaga tu ibilisi
Natamani kwenda kwenu kushtaki
Maneno yako yanafanya ninyong'onye

Sababu nakupenda sana
Ndo maana unafanya visa niumie
Mwenzako bado mi kijana
Nahitaji fursa nipe nitulie

Kamoyo kanaenda mbio
Nakaribia kukata roho
Mwanzako sina kimbilio
Ndo ushanipiga KO

Nipunguzie adhabu basi (Eeeh eeh)
Unipe likizo tu
Mi bado nakupenda mama
Unipe likizo tu
Ona unadhulumu yangu nafsi
Unipe likizo tu
Utaniua mama aaah
Unipe likizo tu

Za chini ya kapeti
Nimepata habari umetolewa posa eh
Inamaana hunitaki umepata
Kibosile kinakupa mapesa (Eeh)
Kwangu ulifuata kiki
Uliishi na mimi kusafiria nyota eeeh
Kweli kisichoridhiki hakiliki
Ona unavyonitesa

Kwenye harusi nitakuja
Nione walivyokupamba mama
Ninajua itaniuma
Ila nitajikaza sana

Nitaleta na zawadi
Nitampa mkono jamaa
Kisha sitokaa sana
Nitaanza ondoka mama

Hali tate nane
Hutaki hata tuonane
Vibaya hivyo
Oh mama, oh tate nane
Unapenda tufokeane
Vibaya hivyo ooh mwana

Nipunguzie adhabu basi, eeh
Unipe likizo tu
Mi bado nakupenda mama
Unipe likizo tu

Ona unadhulumu yangu nafsi
Unipe likizo tu
Utaniua mama, mamaa
Unipe likizo tu

Lalala, lalala lalala
Lalala, lalala lalala

Mola nipe subira, nitampata kisura
Nitaishi na yeye, anipende mwenyewe, mwenyewe
Mola nipe subira, nitampata kisura
Nitaishi na yeye, anipende mwenyewe, mwenyewe

Watch Video

About Likizo

Album : Likizo (Single)
Release Year : 2017
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 03 , 2021

More ASLAY Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl