Mama Lyrics
Mama Lyrics by ASLAY
Mama jamani mama, mama jamani
Mama jamani mama, mama jamani
Natamani nikufuate nikupe hata mkono
Lakini ndo siwezi
Wenye wasiwasi we waziba midomo
Unahitaji pongezi
Kazi yaenda kasi sijaona kikomo
Mama unaupiga mwingi
Hatuna wasiwasi tunalisoma somo
Mama si hatukupigi we
Mama pambana, achana na maneno yatakuchanganya
Visabina zabina ni wengi mama
Hata uwape nini watakusengenya
Binadamu haturidhiki mama Samia
Oooh kazi iendelee
Tupate mapesa na tusherekee
Siku hizi machinga ni mapedeshe
Unapendwa na watoto vijana wazee
Wanakupenda wee
Mama, mama mama, mama Samia Suluhu
Mmemuona mama, mama Samia Suluhu
Rais wetu mama, mama Samia Suluhu
Vigelegele kwa mama, mama Samia Suluhu
Mama kwa kweli unapambana
Kama ni kiu basi we ni maji, twanenepeana
Mama tunakupenda sana
Umewapa nguvu na wawekezaji wanashindana
Mpaka raha
Najivunia kuzaliwa Tanzania
Najivunia pia rais wangu ni Samia
Mama kokoto, mama changanu
Hesabu za bara na pwani zote unazijua
Kila utokapo mi mwenzako nakuombea mama wee
Mama, jamani mama mama jamani
Chochote utakacho inshallah
Mungu atakusimamia mama Samia wee
Mama, jamani mama mama jamani
Oooh kazi iendelee
Tupate mapesa na tusherekee
Siku hizi machinga ni mapedeshe
Unapendwa na watoto vijana wazee
Wanakupenda wee
Mama, mama mama, mama Samia Suluhu
Mmemuona mama, mama Samia Suluhu
Rais wetu mama, mama Samia Suluhu
Vigelegele kwa mama, mama Samia Suluhu
Jana, jamaa, vijana tunapambana
Ndo maana mama atupa fursa sana
Laana laana, tukimdharau mama
Kwa maana mama, hakuna kama mama
Watch Video
About Mama
More ASLAY Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl