Tumekubalika Lyrics
Tumekubalika Lyrics by AMBWENE MWAS ONGWE
Tumekubalika na Mungu tuna nguvu za kifalme
Ametuchora kweli moyoni mwake tu uzao wa agano
Tu uzao mteule aaah aaaaah aaah
Ukuhani wa ki-falmee eeeh aaah aaah
Taifa takatifu aaah aaah oooh ooh
Watu wa milki ya Mungu aaah aaah oooh oh
Nimemwona Mungu amewaleta kutoka
Misri wana nguvu kama za nyati watawavunja adui mifupa
vipande vipande watawachoma adui kwa mishale
yeye kawabariki nani aawalaani Mungu kawabariki
nani wakuwapinga wana nguvuu aaah Mungu kawapa aaah
wanaweza aaah Bwana kawapa aaah oooh
Wanautishoo aaah Bwana kawapa aaah oooh oooh
Hatuwezi tishwa kwa maneno yao nguvu zetu zipo
kwa Bwana aaah tulipona kwa Farao
Tukiwa ugenini hatukufa kwa njaa tukiwa hatuna kitu
Tulinusurika vita tukiwa hatuna silaha tulipona magonjwa
Tukiwa hatuna dawa tulipona ma wifi ndoa zikiwa tetee
Tuliweza maisha tukiwa hatuna hela tulishinda upweke
Tukiwa tumeachwa tuliponywa kesi bila ya mtetezi
Mungu alikuwepo hatukuwa pekee yetu waliotuonea hilo
hawakuja katutoa Misri tuna nguvu kama za nyati kuvunja vipande
katutoa Misri tuna nguvu kama za nyati kuvunja vipande yayaah yaah
Tumekubalika na Mungu
Tuna nguvu za ki-falme ametuchora
kweli moyoni mwake tu uzao wa agano
Usiye lala aaah aah
Usiye lala aaaah aaah
Usiye lala aah aaah aaa
Usiye lala Aaah
Usiwachokoze walio na Mungu wamebarikiwa na
Mungu wakitupwa jangwani wateseke wafe huligeuza bustanii
Tulikula mtama kwa maji tukanawiri kuliko wao hatukupambwa
kama wao tukapendeza zaidi yao walitubadilisha majina hawakubadili
Hatima walipotutupa shimoni tukaibukia Ikulu kule walipotusukumia
ndiko Mungu hupumzikia, walidhani wanatukimbiza kumbe
wanatusindikiza
Watch Video
About Tumekubalika
More AMBWENE MWAS ONGWE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl