UPENDO NKONE Nikae Miguuni Pako cover image

Nikae Miguuni Pako Lyrics

Nikae Miguuni Pako Lyrics by UPENDO NKONE


Ee Bwana Yesu niko mbele zako Baba
Ninakuomba Baba unisikie
Nahitaji nikujue, niyajue maneno yako Yesu
Sheria zako Mungu zikae ndani yangu

Uliwaambia Israeli wazishike sheria zako Bwana
Kusudi baraka zako ziwe juu yangu
Unishike nisipotee nikaenda kwenye njia isiyofaa
Nikaliacha neno likapotea

Unilinde mguu wangu nisifuate mabaya
Adui asinimeze nikaangamia
Huduma yangu mimi, utumishi wangu mimi
Popote napohudumu nikuinue Yesu

Nikumbushe ulikonitoa
Ni mengi umenitendea mimi
Nisije nikasahau wema wako Mungu

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Utusamehe watumishi 
Mara nyingi tumekukosea Baba
Tunavyojiinua na tunakusahau
Miujiza ikitendeka 
Tunasema ni kwa nguvu zetu sisi
Tunasahau kwamba ni wewe umetenda

Tunatumia madhabahu 
Kuyakuza majina yetu sisi
Badala ya kulikuza jina lako Yesu

Tumesahau mapatano
Tulikuahidi ukituinua Baba
Tutakuinua Yesu mataifa wakujue
Hata sisi watumishi
Tumeshindwa kuzifuata amri zako
Tunatamani sana kulirekebisha neno

Na kama ungeturuhusu 
Tuweze kulirekebisha neno
Kila mtu angejiongoza anavyotaka yeye
Tunafanya mazingaombwe

Kwenye madhabahu yako Yesu
Tunadhani tunaweza kukusaidia Mungu
Tunapiga sarakasi nyingi
Madhabahuni pako Baba
Tunadhani tunaweza kukusaidia Mungu

Lakini mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Mimi nikae miguuni pako
Ninaomba Baba unifundishe 
Roho wa Mungu mwalimu mwema
Ninaomba Baba unifundishe 

Watch Video

About Nikae Miguuni Pako

Album : Nikae Miguuni Pako (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 16 , 2021

More UPENDO NKONE Lyrics

UPENDO NKONE
UPENDO NKONE
UPENDO NKONE
UPENDO NKONE

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl