Uswazi Lyrics
Uswazi Lyrics by BANDO
(Wamemchokoza Bear!)
Karibu Uswazi takeaway
Karibu homeboy tunaishi giza
Na mtaa unaitwa Makoroboi
Usijione mshamba
Kuwashangaa maisha ya mjini
Huku mchana fundi kitanda
Alafu usiku analala chini
Uswazi kwetu
Sometime kuna mambo ya kiwaki
Boda boda wali chipsi
Ila anapakia mishikaki
Njoo uone mabafu mafupi my dear
Unaeza kuwa unaoga huku ukimtongoza mpita njia
Hawajui kupenda madada wanajali kesho
Rais aliyegundua mapenzi naye alikufa kwa space
Kifupi mtaani kwetu mapenzi bado machungu
Ukiitwa mpenzi bila pesa we ni mpenzi wa Mungu
Machizi kula unga since wamebugi ramani
Hata chuo kina wajinga ndio maana kuna mtihani
Ukiwa ndezi utapakatwa na muwa
Dem wako asipouona mwezi ujue amepatwa na jua
We mtoto tulia, tulia tulia tulia
Wapi umekulia, kulia kulia kulia
Hayo mawenge na mapepe
Mtaani kwetu huku usilete
Bando anasukuma kete
Shua twende, weka tuweke
Mahitaji si utani ila mtaani tumehalalisha
Yaani kila dem mzuri tayari tumemzalisha
Ndo maisha ya nyumbani
Mganga anaweza akawa na dawa zote
Ila ya meno akanunua dukani
Kwetu bomba kupambana ndo tunaamini ulijali
Mambo yanasonga ila hayawezi kusonga ugali
Machizi kila mchongo yanakimbizwa dube dube
Na naamini kwamba milioni pesa laki ni dube
Wahuni tukiamka asubuhi mswaki ndo fegi
Hadi mtendaji wa kata ana degree ya ulevi
Tunachokipata tunashare kila kwanja
Roho mbaya haijengi maana roho mbaya haina kiwanja
Na sisi ni watoto wa shangazi
Kila muda ni starehe
Tushachukiwa na wazazi
Kabla hata hatuja baleghe
Kwa iyo ukileta chuki kwetu easy
Maana kelele za mlango
Hazimnyimi mwenye nyumba usingizi
We mtoto tulia, tulia tulia tulia
Wapi umekulia, kulia kulia kulia
Hayo mawenge na mapepe
Mtaani kwetu huku usilete
Bando anasukuma kete
Shua twende, weka tuweke
Hali ya kwetu napotoka sio shwari
Yaani Kijito Nyama, Sinza mchicha
Makumbusho ndo ugali
(Kiri Records)
Let's take over the game
Watch Video
About Uswazi
More BANDO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl