UPENDO WISDOM K Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times) cover image

Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times) Lyrics

Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times) Lyrics by UPENDO WISDOM K


Mungu wa nyakati zote, nakuabudu
Mungu wa wote wenye mwili, nakuabudu
Mwenye mamlaka yote, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Mungu unayeishi, nakuabudu
Mungu unayejibu, nakuabudu
Mzee wa siku, nakuabudu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Milimani mabondeni, gizani nuruni
Kiangazi au masika Kwenye raha au majonzi
Mkono wako waokoa, roho wako wafariji
We ni Mungu wa nyakati zote

Haulinganishwi na chochote
Hautetemeshwi na majira
Ulikuwako sasa uko na milele
Na milele utadumu

Alpha Omega mwanzo mwisho
Watangaza mwisho kabla ya mwanzo
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Ee Mungu mwenyezi, nakuabudu
Mungu mwenye enzi, nakuabudu
Mshika maagano, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu

Mungu mtukufu, nakuabudu
Mungu mtakatifu, nakuabudu
Mungu mkamilifu, nakuabudu
Uweza wako ni wa ajabu

Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wastahili Bwana, wastahili Bwana
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Unaweza Bwana, unaweza Bwana
Uweza wako ni wa ajabu

Yesu uweza wako ni wa ajabu
Wewe ni Mungu wa nyakati zote

Watch Video

About Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times)

Album : Mungu wa Nyakati zote ( God of all Times)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Apr 07 , 2020

More UPENDO WISDOM K Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl