Ankula huu Lyrics
Ankula huu Lyrics by SANAIPEI TANDE
Alikua yuanipenda hapo zamani alipokua Hana
Na kile tulichopata ingawa haba tulikigawanya
Akapandishwa cheo maendeleo akaanza kunikaana
Akapata ndongo ndongo na mimi akanipa kisogo
Ikawa kwangu makelele kwake starehe
Kwangu matusi kwake mazuri
Nashaanga Leo yuaniomba msamaha
Yuanimbembeleza yuanitendekeza yuaninyenyekea mimi
Nami sitodhubutu kumruhusu anihusu tena
Ankula huu
Na hasara juu
Nilipoyangundua nikamuonya awachane nae
Akaniona punguani akanivalia mi miwani
Lakini mambo kaenda mrama bibi akaanza kutanga
Leo yuashika tamaa huku akiniandama
Ikawa kwake makelele kwangu starehe
Kwake matusi kwangu mazuri nashaanga Leo yuaomba msamaha
Yuanimbembeleza Yuanitendekeza yuaninyenyekea mimi
Nami sitodhubutu kumruhusu anihusu tena
Ankula huu
Na hasara juu
Wanasema kosa ni la kwanza
Mara ya pili ni kwa madharau
Ikiwa ntakurudia bwana
Nakusihi usinbwage bwaya bwaya
Watch Video
About Ankula huu
More SANAIPEI TANDE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl