RAPCHA 40 Missed Calls cover image

40 Missed Calls Lyrics

40 Missed Calls Lyrics by RAPCHA


Someone is playing with me
Kuna mtu ananichezea
Someone is playing with me
Nashuka kiuchumi ndoa yangu inachafuka
Kuna mchezo unaendelea they are playing with me
Muda mchache kwenye ndoa maumivu yamenizidia
Huu ni mwezi wa tano unaingia
Nkitazama muda ni Saa sita usiku
Baada ya kumtafuta sana
Huyu mwenzangu ndo nyumbani anaingia
Niambie umetoka wapi salma
Hii kesi isidingo si tumetoka kuisolve jana
Isingefika 40 missed calls ka ulikua kwa mama
Nakuambiaga huniheshimu Salma unanidharau sana
Story zako mjini naambiwa
Hamna kitu kinaniuma kama habari kwamba mi namegewa
Unanipandisha hasira
Navokuambia ukweli afu unanijibu kwa kufoka
kama unaonewa Hebu Leta simu yako, fungua
Salma usinipandishie, icho kiburi chako ntakupasua
Naichukua nianze kuipekua akaja kuikwapua
Akili ikaflip, gun nkanyanyua
Salma Kanijia juu, Nimechoka maisha ya kubaniwa
Bora tu tuachane umezidi kunitishia
Story za malaya wako nikikuambia unajifanya mkali
Kama we kidume fyatua
Gun shots

Nilikupenda mpaka kufuru
Nikawa nawaza jidhuru
Ukiwa mbali
Tena nikakupa uhuru
Na ukashindwa shukuru
Ikawa ndo dosari
Ukaenda ku date na wale
Mi wakuwa nasota we ule
Na mie kukuacha siwezi
Ni bora dunia tuiache aah

Fahamu zinarudi akili imeduaa
Salma anateseka chini baada ya risasi nne kumvaa
Hofu kubwa inaniingia nikiangalia
Damu yake inavyonililia chini inatapakaa
Ndo Idea ya kukamatwa ikanijia
Nikajua haitopita muda mapolisi watanitimbia
Ila nguvu zote zishaniishia

Nikiumia kuona safari yetu ya mapenzi ilipokwamia
Dhambi inaanza kunitafuna
Natamani nirudishe muda nyuma niongee na Salma
Najiona mnafki kwa kumwaga damu
kwa makosa ambayo moyoni najua kuwa na mimi nafanya
Itanitesa maisha yangu yote hii memory
Ego zetu zimefanya tumeharibu destiny
Vita na Insecurities hakukuwa na honesty
Na loyalty marafiki wakatunyima privacy
Litimie agano
Nahisi Mungu ametuchagua mi na wewe tuwe mfano
Salma, hukustahili hii adhabu ninakiri
Naomba kabla haujafika mbali nisubiri

Roho yangu inauma
Kosa lako kuzichezea hisia zangu Inamaana hukuona
Nilivyopambana kuziheshimu hisia zako? Aaah

Nilikupenda mpaka kufuru
Nikawa nawaza jidhuru
Ukiwa mbali
Tena nikakupa uhuru
Na ukashindwa shukuru
Ikawa ndo dosari
Ukaenda ku date na wale
Mi wakuwa nasota we ule
Na mie kukuacha siwezi
Ni bora dunia tuiache aah

Watch Video

About 40 Missed Calls

Album : To The Top Vol 2 (Album)
Release Year : 40
Added By : Farida
Published : Jul 18 , 2023

More RAPCHA Lyrics

Low
RAPCHA
ICU
RAPCHA
RAPCHA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl