Don't Cry Lyrics
Don't Cry Lyrics by ONE SIX
Mama don't cry
One Six the one tell you
Yeii ye eeh
Kuishi duniani napo pia kwetu karama(Aaah)
Nayatambua maumivu yako mama(Aaah)
Usihuzunike na kusema ameamua kuchukua wako tu
Ni mapito ya dunia ma, mapito ya dunia
Uliamini wampa kondoo wakombozi(Aaah)
Mshahara kwake schoolfees ulilipa
Wakati mwingine hata njaa nililala
Ukidhani nyumba utaleta mabigiri
Hey my mama don't cry
Muombee Jacky atasimama
Pengine ni majaribu
Kumpoteza junior wako inauma
Hey my mama don't cry
Muombee Jacky atasimama
Pengine ni majaribu
Kumpoteza junior wako inauma
Mziki umepoteza ndoto za mwanao ooh no no
Ridhiki hakufanikiwa kuwa nao
Alitaka kuwa doctor alitaka kuwa rubani
Alitaka kuwa nahodha
Junior kupoteza alipoanza kuimba
Shule kupuuza kwa kupenda muziki
Ulimbembeleza aiwe mwanamuziki mama
Hakusikiliza akasema mama niacha mama niache
Matokeo yake kakwachia simanzi
Kuanza kuvuta sigara na mabangi
Hata pombe nazo pia alitamani
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi
Mungu ni wa wote mama
Usihuzunike moyo ooo
Pole mama Junior wee
Eeh eeh eeeh
Yo my mama don't cry
Nafahamu kwamba wazazi wengi sana
Waliosomesha watoto wao kwa gharama nyingi
Walijinyima wakati mwingine hata kula
Walilala njaa na watoto wao waikiamini kwamba
Elimu ndio ufunguo wa maisha
Elimu ndio itakayoleta ukombozi katika familia
Na hata mzazi akizeeka asaidiwe
Matokeo yake wa kina mama zetu ambao wametuzaa
Matumaini yao kuwa tunawaachia maumivu
Baada ya kuingia kwenye shughuli ambayo
Ukiamini inakutoa lakini shughuli hiyo kuna mawili
Kuna pata potea, ni kama kamari namaanisha ni muziki
Ambayo ukiamua kuingia kuna mafanikio au pia unaweza
Kupata mafanikio hayo hayo ukayachezea
Lakini pia unaweza usipate mafanikio ukapoteza muda
Pole sana...
Ndoto za kuwa rubani
Kutaka kuwa mwalimu
Wenzake awafundishe
Ulitamani awe doctor
Hata angekuwa nahodha
Mameli atuendeshe
My mama don't cry mama
Ongeza kusali sana
Atabadilika Junior
Mungu yupo anamwona
Eeeh mama don't cry yayayaya
Ah wako Junior
Hey my mama don't cry
Muombee Jacky atasimama
Pengine ni majaribu
Kumpoteza junior wako inauma
Hey my mama don't cry
Muombee Jacky atasimama
Pengine ni majaribu
Kumpoteza junior wako inauma
Watch Video
About Don't Cry
More ONE SIX Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl