Nitabadilika Lyrics
Nitabadilika Lyrics by MR BLUE
Nikitoka tungi, nikirudi tungi
Nguvumbi mdomoni kutu na merungi
Kete na makundi vicheche sijivungi
Siku inaishaga bar nikilala kila ukumbi
Alfajiri ikifika ndo narudi
Nimekasirika nimekunja ndita
Sorry mama sipendi kukuudhi
Mambo ya ujana na nitabadilika
Kabla ya kulala napiga goti kwa Allah
Kila siku ni sala kuiombea hii familia
Namwomba Mola hili kapu litie fora
Nyumbani maisha bora na ndani wainuke bora
Mimi ni binadamu mama sijakamilika
Hizi kero ndogo ndogo sawa nitabadilika
Najua unanijua lile penzi nalokupa
Zawadi yako ni mimi usinuitenge kisa chupa
Nachopata ni kidogo ila chote nakupa wewe
Nakutunza kwa chakula na ukitaka pombe ulewe
Vumilia hii tabia hela zote nakunywa bia
Kuna siku nitatulia na masikio yatakusikia
Koma na mimi
Shida ndogo ndogo nisitiri
Kwa kulea watoto ni mimi nawe
We na mimi
Koma na mimi
Shida ndogo ndogo nisitiri
Kwa kulea watoto ni mimi nawe
We na mimi
Muda wake ni kidogo tu
Muda mwingi marafiki
Muda mwingi kwenye mziki
Muda kutafta riziki
Muda kutafta makiki
Muda wa kumtafuta shabiki
Muda(Muda)
Awali haikuwa hivi
Rafiki wananiuliza kheri umekuwa chizi?
Na mimi ndo nawajib, Mbona mnakuwa hivi?
Hamjui kama chizi hajijui akiwa chizi?
Hata nikupe malazi makasi
Lazima utatafuta penzi letu lilipo
Na mi ninakuweka wazi
Sheria ya kwanza ni harusi na inayofuata ni kifo
Ibilisi na shetani umeniganda
Umenifanya kama gasi mtoto wa watu unanipanda
Ona nananana nitakutwa kutwa kwenye ubanda
Shemeji mchawi, mke namwona mwanga
Kama kuna jitu limeniendea kwa mganga
Dah! Mi mwenyewe naumia
Ita bia hela zote nakunywa bia
Kuna siku nitatulia, na masikio yatakusikia
Koma na mimi
Shida ndogo ndogo nisitiri
Kwa kulea watoto ni mimi nawe
We na mimi
Koma na mimi
Shida ndogo ndogo nisitiri
Kwa kulea watoto ni mimi nawe
We na mimi
Nitabadilika, nitabadilika
Nitabadilika, nitabadilika
Watch Video
About Nitabadilika
More MR BLUE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl