Ya Uchungu Lyrics

MARIOO Tanzanie | Bongo Flava,

Ya Uchungu Lyrics


Wakisema tutaachana
Ongeza nipenda zaidi ya jana
Wakitamani tuhuzunike
Tufanye sherehe

Baby nipe tena kama jana
Wanatamani yanibubujike
Ukinitenda kiutani utani
Utaniua eeh

Mi juu yako nishatamba sana
Nitaambia nini watu?
We ndo faraja maishani 
Usiniue eeh
Milele kufa kuzikana 
Nishachora na tattoo

Hata ukiniacha 
Usifanye ukatoka na kina niniii
Hii hii hii 
Nitaificha wapi sura
Utanitia doa

Hata ukiniacha 
Vya ndani ibaki siri 
We nami, Eeeh eeh eeeh
Nitaiweka wapi sura
Nitaiona dunia

Ya uchungu
Ya uchungu
Ya uchungu
Ya uchungu

Achana na mapaka shume
Wataponza uchomoe
Wasije wakakufunza
Unikomoe

Wala hawatakuwa na maana
Lengo penzi walibomoe
Lazizi wee, basi fanya
Usiniboe 

Maana moyo wangu utaumia
Utaumia aah
Alafu nafsi yangu itajutia 
Itajutia

Hata ukiniacha 
Usifanye ukatoka na kina niniii
Hii hii hii 
Nitaificha wapi sura
Utanitia doa

Hata ukiniacha 
Vya ndani ibaki siri 
We nami, Eeeh eeh eeeh
Nitaiweka wapi sura?
Nitaiona dunia

Ya uchungu
Ukiondoka ukiniacha mwenzako nitaumia
Ya uchungu
Itanielemea, itaniua sana

Ya uchungu
Maradhi ya mapenzi nayo yanaumiza sana
Ya uchungu
Mwenzako aah, eeh eeh

Mwenzako napenda 
Napenda vibaya
Ukiniacha nitaumia
Ukiondoka nitaumia

MARIOO (19 lyrics)

Marioo is a Tanzanian singer/songwriter  based in Dar Es Salam. His first single (Dar Kugumu), recorded in 2017, became very popular and hit a number one song almost in all radio stations in Tanzania.

Leave a Comment