Nisamehe Lyrics by KALA JEREMIAH


Nakiri nilikuumiza sana mama yangu
Nyumbani kukugonganisha na machangu
Pia kukugombanisha na ndugu zangu
Ili mradi nifurahi ndani ya nafsi yangu

Nakunywa ninalewa na rafiki zangu
Nakuangushia kipigo na una mimba yangu
Mpaka mimba ikachoroboka kwa ujinga wangu
Leo nitaficha wapi mimi sura yangu?
Mbele sioni kitu zaidi ya ukungu
Na maadui wako wengi zaidi ya nywele zangu

Nishike mkono mikosi inaniandama
Na usipo nionea huruma haki ya nani nitazama
Mwili hauna nguvu kama mwenye homa
Nahisi niko kuzimu na shetani ananichoma
Ongea chochote na nafsi yangu itapona
Nakiri sitorudia tena mbele ya Maulana

Najua unanisikiaaa 
Ila kunijibu ndo huwezi
Eeeh Mungu baba saidiaaa 
Umlaze mahala pema mpenzi
Na pia anisamehe maha, anisamehe
Na pia anisamehe sana, anisamehe

Nisamehe nitakufa, kwa mawazo ya msongo
Wapambe walionipamba, wamenigeuzia mgongo
Baada ya kuishiwa pesa, wanadai sina mpango
Ni kweli sina dini, wala sina mchongo
Siku hizi sinywi bia, ni viroba mixer gongo

Nisikufiche, nimepoteza malengo
Kwenye kupa kwa mizigo, kwenye lori mi ndio tingo
Maisha yangu yanaelekea ukingo
Na kama nitakufa leo, jua kuu uliacha pengo

Nikiongea sana nikajitukana
Maana nilifungwa macho na starehe za ujana
Nikajiita pimpi kicheche bonge la bana
Nikakupa mateso ya moyo, mwili kimwana
Na kila nilipolewa ni kichapo cha kufana
Nishike mkono japo nimelewa sana
Sema neno moja liuponye mwili wenye laana

Najua unanisikiaaa 
Ila kunijibu ndo huwezi
Eeeh Mungu baba saidiaaa 
Umlaze mahala pema mpenzi
Na pia anisamehe maha, anisamehe
Na pia anisamehe sana, anisamehe

Nakiri sina uti, ila sasa nakwangukia
Unanijua vizuri, sina haja ya kuhadithia
Ila sirudii makosa haki ya Mungu naapia
Sauti za kuzimu ninazisikia
Bila msamaha wako hakika nita disappear
Mi kipofu niongoze, natanga sioni njia

Nakiri mi ni bonge la fala tena mburula
Nilikuona taka-taka nikazurura
Nikapiga chaka kwa chaka na kina Shura
Sasa cheki nilivyo, nimenyooka kama rula
Natamani ardhi ipasuke nijifiche sura

Ama kweli dunia imenielemea
Mzigo ni mzito Golgotha naelekea
Ndugu wa damu yangu, sioni walikoelekea
Hakika ni wewe pekee unaweza kunitetea
Nadhani sasa sina tena cha kuongea

Najua unanisikiaaa 
Ila kunijibu ndo huwezi
Eeeh Mungu baba saidiaaa 
Umlaze mahala pema mpenzi
Na pia anisamehe maha, anisamehe
Na pia anisamehe sana, anisamehe

Watch Video

About Nisamehe

Album : Nisamehe (Single)
Release Year : 2019
Copyright : All rights to the owner.
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jun 08 , 2019

More KALA JEREMIAH Lyrics

KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl