R.I.P JPM Lyrics
R.I.P JPM Lyrics by K2GA
Tanzania mmmh
Ni wewe, shujaa wetu
Ni wewe, mjasiri wetu
Ni wewe ulotupa nuru watanzania
Komanda wetu
Ni wewe, shujaa wetu
Ni wewe, mjasiri wetu
Ni wewe ulotuonyesha njia watanzania
Komanda wetu
Umetutoa kwenye kiza
Ukatuvuta mikono ukatuleta kwenye taa
Na ukatukogesha sasa twapendeza tena tunang'aa
Miaka mitano ikapita, na mengine tukakupa we
Imani yetu furaha yetu ukiongoza Tanzania
Ulipokuja ulituambia hapa kazi tulisisitizia
Umeondoka umetuacha kimya kimya hata kutuambia
Bendera imetulia wananchi tunakulilia wee
Viongozi wamejiinamia hatuna la kufanya Mungu kashaamua
Ni wewe aah, ni wewe uuh
Ni wewe Magufuli tunakulilia
Baba ni wewe, ni wewe uuh
Ni wewe kweli umetuacha peke yetu Tanzania
Tulikuita chuma, shujaa
Mkombozi wa wanyonge
Tena uliweka njia pasipokuwa na njia
Viongozi wa bongo majibu ukayatuma
Ukaweka nguvu ipate kukua
Hakuna kama wewe nani asiyekujua
Hivi mnakumbuka juzi tu Dodoma aliapa
Kwamba atashika miaka mitano tulompatia
Ndo kwanza miezi sasa hata mwaka mmoja hujafika
Mama Samia ametangaza Rais Magufuli ametangulia
Ni wewe aah, ni wewe uuh
Ni wewe Magufuli tunakulilia
Baba ni wewe, ni wewe uuh
Ni wewe kweli umetuacha peke yetu Tanzania
Watch Video
About R.I.P JPM
More K2GA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl