Nafasi Nyingine Lyrics
Nafasi Nyingine Lyrics by JOEL LWAGA
Mavumbi umenifuta yote
Habari umebadili yote
Machozi umenifuta yote
Aibu umeondoa yote
Umeniita mwana niliyekuwa mtumwa
Umenisimamisha katika wingi wa neema
Na umeniketisha mahali pa juu sana
Ninaucheka wakati uliopita
Nikiufurahia ule ujao
Ninaucheka wakati uliopita
Nikiufurahia ule ujao
Maana umenipa(Nafasi nyingine)
Umenipenda tena bila kukoma(Nafasi nyingine)
Neema yako imeniinua tena(Nafasi nyingine)
Umenipa tena bila kuchoka(Nafasi nyingine)
Mungu wa neema
Wa neeema(Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Madaktari walisema sitapona tena
Walimu walisema nitafeli
Ndugu na jamaa walisema nimeshindikana
Na kumbe wewe waniwazia mema
Umri uliposogea walisema ndoa si fungu langu
Nilipofiwa na mpendwa yule walisema sitaweza tena
Baada tu ya kufilisika, sikumwona wa kuniombea
Na kumbe ndani yao walifurahi niliyopitia
Ninaucheka wakati uliopita
Nikiufurahia ule ujao
Ninaucheka wakati uliopita
Nikiufurahia ule ujao
Maana umenipa(Nafasi nyingine)
Umenipenda tena bila kukoma(Nafasi nyingine)
Neema yako imeniinua tena(Nafasi nyingine)
Umenipa tena bila kuchoka(Nafasi nyingine)
Mungu wa neema
Wa neeema(Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Maana umenipa(Nafasi nyingine)
Kweli umenipa(Nafasi nyingine)
Umenipa(Nafasi nyingine)
Bwana umenipa(Nafasi nyingine)
Mungu wa neema
Wa neeema(Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Wa neema, neema (Aaah)
Watch Video
About Nafasi Nyingine
More JOEL LWAGA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl