
Muda Lyrics
...
Muda Lyrics by JOEL LWAGA
Ni kweli
Naonekana niko nyuma
Kila kukicha watu washamiri
Kwa magai majumba
Juzi juzi
Wengine tulikuwa nao sawa tu
Ila kwas asa si wenzangu tena
Siwagusi hata nukta
Ni kama niko duniani kuwasindikiza wao
Usipotulia unaweza sema
Mungu ni wa peke yao
Ila maisha ni kama foleni
Inajongea mdogo mdogo
Mungu wao ndio mungu wangu
Ndio wa isaka na yakobo
Wakati na bahati, huwapata wote
Zamu yangu itafika, wacha niliongejee
La maana ni uhai
Mungu ni wote
Ndio anapanga aanze nani, nani afuate
Yani ni suala la muda (muda)
Nipeni tu muda
Mungu ni wa wote jamani
Muda nipeni tu muda
Yani ni suala la muda (muda)
Nipeni tu muda
Kikubwa niko kwa foleni
Muda nipeni tu muda
Aaah aaah
Najua wengi husema
Kila asiyenacho huyenyekea
Ila nimemwomba mungu
Nisibadilike akinipea
Vile nawaona watu, na kuwachukulia nikiwa sina
Nisije jiona mungu mtu
Pindi mambo yakininyookea
Najitahidi kugawana hichi kidogo
Nilichonacho na wenzangu
Nimejifunza kwamba kutoa ni moyo
Moyo sio mpaka kiwe kingi changu
Kwenye sadaka sinaga visingizio
Hio ni kama pai kwangu
Hata nikiwa sina kabisa siku hyo
Mungu anaujua moyo wangu
Wakati na bahati huwapata wote
Zamu yangu itafika, wacha niliongejee
La maana ni uhai
Mungu ni wote
Ndio anapanga aanze nani, nani afuate
Yani ni suala la muda (muda)
Nipeni tu muda
Mungu ni wa wote jamani
Muda nipeni tu muda
Yani ni suala la muda (muda)
Nipeni tu muda
Kikubwa niko kwa foleni
Muda nipeni tu muda
Yani ni suala la muda (muda)
Nipeni tu muda
Mungu ni wa wote jamani
Muda nipeni tu muda
Kikubwa niko kwa foleni
Muda nipeni tu muda
Mungu ni mwaminifu
Muda nipeni tu muda
Maana maisha ni foleni
Kila siku inatembea pole pole
Namwamini mungu ipo siku nitafanikiwa
Maana maisha ni foleni
Kila siku inatembea pole pole
Namwamini mungu ipo siku nitafanikiwa
Kweli ni suala la muda
Muda nipeni tu muda
Mungu ni mwaminifu jamani
Muda nipeni tu muda
Watch Video
About Muda
More JOEL LWAGA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl