Maneno Mazuri Lyrics by JAPHET ZABRON


Mmekata kusimulia mema wangu mimi 
Japo mwayajua mmenyamaza 
Mko tayari kuelezea ubaya wangu mimi
Ili nafsi zenyu zifurahi

Mmekata kudhibitisha yupi mwenye haki
Japo mwamjua mmenyamaza
Mko tayari kumpoteza mtu nafsi yake 
Ili nafsi zenyu zifurahi

Mliyahesabu makosa ya mtu 
Mkaacha wema nilowatendea 
Wala hamjali ntaumia vipi 
Kwa kauli zenu mlizosema 

Mwanenee watu wenu maneno mazuri 
Mwabariki kwa usemi uko mtaani 
Wanapopatwa matatizo uumie nao 
Na wakati kuna mazuri mfurahi nao 

Furahi pamoja na wanaofurahio 
Lieni pamoja na waliao 
Mkubali kushugulishwa
Na mambo manyonge 

Msiwe wa kujivuna akili
Msimlipe mtu ovu kwa ovu 
Anagalieni yaliyo mema
Machoni pa watu wote 

Chozi la aliaye kwa mwenye huzuni lina thamani
Kuliko cheko la achekaye na achakaye
Aijuaye huzuni la mnyonge humaanisha 
Kuliko achekaye na mwenye furaha 

Mwanenee watu wenu maneno mazuri 
Mwabariki kwa usemi uko mtaani 
Wanapopatwa matatizo uumie nao 
Na wakati kuna mazuri mfurahi nao 

Msiba wa mtu sifa nzuri zitazungumzwa
Ni siku pekeee, husemi kwa ubaya
Mwambieni mtu wema wake bado yuko hai
Mwonyeshe upendo mfurahi naye

Watch Video

About Maneno Mazuri

Album : Maneno Mazuri (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 17 , 2021

More JAPHET ZABRON Lyrics

JAPHET ZABRON
JAPHET ZABRON
JAPHET ZABRON
JAPHET ZABRON

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl