Nipe Lyrics by GOODLUCK GOZBERT


[VERSE 1]
Hata nikiwa sina chakula
Isinifanye kusahau
Ulinilisha nikasaza
Hata nikiwa sina mavazi
Isinifanye nikufuru
Nakusahau umeniweka hai

Ona wapo marafiki
Wanakosa kula na kuvaa
Hawalalamiki wanakushukuru tu
Mimi eeh, nilikupa nini Baba
Cha kunipa kibali
Kwa siku zilizofurahisha

Tabu kidogo zisifanye nikusahau
Umeshatenda mengi nikiwa hapa
Eeh! Shida itapita bado kidogo
Ikiwa nitachoka ninue

[CHORUS]
Nipe ... (Kukumbuka wema)
Ooh Nipe... (Kumbuka wema)
Aahh Nipe (Kumbuka wema)
Nipe… Wako…


Nipe ... (Kukumbuka wema)
Nipe... (Kumbuka wema)
Ooh Nipe... (Kumbuka wema)
Oooh… Wako ooh…

[VERSE 2]
Hata kwenye bonde hili la mauti
Nakumbuka nilikuita
Na wewe ukaitika, Baba
Kutegemea akili zangu
Na mawazo Yangu…
Kutanifanya niendelee
Ah niendeleee kulalamika
Kuna kipindi najisahau
Na kujivunia mafanikio
Wengine naona taka taka. Eh!
Nikumbushe mi ni MTU tu
Na dunia tunapita
Uhai wangu si faida bila wewe

Mungu Wewe nii mkuu
Kuliko vile nakutazama Baba
Unisamehe unisamehe
Kuna nyakati nadhani
Hii dunia labda ni ya ushindani
Natumia akili Zangu za ndani
Ila bado nashindwa kuendelea
Nikumbushe nisidhani
Wakifanikiwa tuna upinzani
Nifundishe kuwaombea amani
Na utatenda kwa wakati

[Bridge]
Na ikiwa kama Nikisahau
unikumbushe mi mtoto wako
Kama nikisahau
Unikumbushe mi mtoto wako

[CHORUS]
Nipe ... (Kukumbuka wema)
Ooh Nipe... (Kumbuka wema)
Aahh Nipe (Kumbuka wema)
Nipe... Wako…

Nipe ... (Kukumbuka wema)
Ooh Nipe... (Kumbuka wema)
Ooh Nipe... (Kumbuka wema)
Ooohoo… Wako…

Oh wewe wewe (kumbuka wema)
Kumbuka wema… Kumbuka wema… Wako..

Hata nisipofanikwa (Kumbuka wema)
Nikarudi kwenye dhiki (Kumbuka wema)
Kupoteza marafiki (Kumbuka wema)
Unikumbushe kumbushe tu (wako)
Baba Yangu (Kumbuka wema)
Ooooh Nikumbuke pia (Kumbuka wema)
Oooh fadhili zako (Kumbuka wema)
Unikumbushe Jehova (Kumbuka wema)
Unikumbushe Masihi (Kumbuka wema)
Kwamba uliniumba niwe (Kukumbuka wema)
Vile utakavyo oooh wakoo ooh

 

Watch Video

About Nipe

Album : SHUKURANI (Album)
Release Year : 2018
Added By : Afrika Lyrics
Published : Aug 26 , 2018

More GOODLUCK GOZBERT Lyrics

GOODLUCK GOZBERT
GOODLUCK GOZBERT
GOODLUCK GOZBERT
GOODLUCK GOZBERT

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl