Nibadilishe Lyrics

GOODLUCK GOZBERT Tanzanie | Gospel,

Nibadilishe Lyrics


Kwanza nimenyoa deni
Napenda sana mitindo ya nywele
Kuruka usiseme 
Viwanja vipya ninakaribishwa

Kwenye kura saa za Insta nakesha
Nikitafuta tena mabaya
Nikisikia mabata nataka
Nalitafuta tena nalipa

Wala silipi maden, Nikikopa na beti
Wala sionagi soni
Fungu la kumi kwangu hio ni stori
Nasubiri jumapili(Sunday)

Hata najua sina imani, japo naitikia Amina
Nasubiria ukitendaga kwanza, ndio nikubali
Aah kama Yesu najua na idadi ya vitabu najua 
Na yalipo makanisa najua, ila kuhudhuria nashindwa

Oooh kwa ibada nasinzia, sijui mdudu kaingia
Ila nikiona bia, nasikia kuchangamkaa
Oooh kwa ibada nasinzia, sijui mdudu kaingia
Ila nikiona bia, nasikia kuchangamkaa

Eeh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe
Oooh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe

Kuna venye hii movie inanichoma 
Hasa ile parapanda
Ikipigwa wakizika
Na appear, sirudii kosa

Maneno yananichoma
Binadamu ni maua
Ikipita wiki moja masikini
Nasahau kabisa 

Oooh kwa ibada nasinzia, sijui mdudu kaingia
Ila nikiona bia, nasikia kuchangamkaa
Oooh kwa ibada nasinzia, sijui mdudu kaingia
Ila nikiona bia, nasikia kuchangamkaa

Eeh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe
Oooh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe

Nakupa maisha na moyo, utakase
Ninapoanguka nishike nisimame 
Nakupa maisha na moyo, utakase
Ninapoanguka nishike nisimame

Eeh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe
Oooh niko na ubaya, niko na ubaya
Eeh niko na ubaya, Bwana nibadilishe

Leave a Comment