ZABRON SINGERS Usiniache  cover image

Paroles de Usiniache

Paroles de Usiniache Par ZABRON SINGERS


Sitaki kuwa wa hivi hivi mimi
Kuipenda dunia nikaikosa mbingu
Kuwa vumbi la majivu kwa watakatifu
Litakalo kanyagwa na wa washindi wa dhambi

Sitaki kuwa wa hivi hivi mimi
Kuipenda dunia nikaikosa mbingu
Kuwa vumbi la majivu kwa watakatifu
Litakalo kanyagwa na wa washindi wa dhambi

Duniani mbinguni Mungu tuwe wote
Mbali ulikonitoa usiniache
Na ukiwa umeniheshimisha hapa chini
Yesu akija ruhusu niende na yeye

Ninafurahi kuona vile unanijali
Nikiwa mdogo mkubwa Mungu uko nami
Kwenye vikwazo vitisho umekuwa na mimi 
Mchana usiku bega kwa bega uko nami

(Eh usiniache Mungu wangu)
Baba tangu nikiwa mdogo mdogo umekuwa nami
Siku zote
(Umenibariki vingi, ukanisamehe mengi)
Baba ukinibariki unikumbushe nisikusahau
Siku zote

(Nia yangu mi unimiliki baba yangu jana, leo)
Baba na mpango kwenda Jerusalem
Unikumbuke niwe pale
Usiniache Mungu wangu (Baba)
Usiniache Mungu wangu (Baba)
Usiniache  (Baba) Siku zote

Umenibariki vingi (Baba) 
Ukanisamehe mengi (Baba) 
Usiniache (Baba)

Nia yangu Mungu (Baba)
Unimiliki baba yangu (Baba)
Jana leo hata kesho (Baba)

Lutu alikataa kubaki hivyo hivyo
Ukakataa kupenda uovu wa Sodoma
Katikati ya mji wa uovu wa dhambi
Kwa uaminifu ukamuakilisha Mungu

Lutu alikataa kubaki hivyo hivyo
Ukakataa kupenda uovu wa Sodoma
Katikati ya mji wa uovu wa dhambi
Kwa uaminifu ukamuakilisha Mungu

Naomba nami niwe mtumwa mwaminifu
Niwakilishe vyema jina la Yesu
Hata kama dunia ikidhiri uovu
Ruhusu nisimame nikutetee

Na siku ile Mwokozi wangu ataporudi
Aseme vyema we ni mtumishi mwema
Kisha nikae nipae mawingu nina Yesu
Kuanzisha familia mpya na Mungu

(Eh usiniache Mungu wangu)
Baba tangu nikiwa mdogo mdogo umekuwa nami
Siku zote
(Umenibariki vingi, ukanisamehe mengi)
Baba ukinibariki unikumbushe nisikusahau
Siku zote

(Nia yangu mi unimiliki baba yangu jana, leo)
Baba na mpango kwenda Jerusalem
Unikumbuke niwe pale
Usiniache Mungu wangu (Baba)
Usiniache Mungu wangu (Baba)
Usiniache  (Baba) Siku zote

Umenibariki vingi (Baba) 
Ukanisamehe mengi (Baba) 
Usiniache (Baba)

Nia yangu Mungu (Baba)
Unimiliki baba yangu (Baba)
Jana leo hata kesho (Baba)

Ecouter

A Propos de "Usiniache "

Album : Usiniache (Single)
Année de Sortie : 2021
Copyright : (c) 2022
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Jan 09 , 2022

Plus de Lyrics de ZABRON SINGERS

ZABRON SINGERS
ZABRON SINGERS
ZABRON SINGERS
ZABRON SINGERS

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl