Paroles de Nenda
Paroles de Nenda Par MACVOICE
(Ayolizer)
Mmmh siri ya mwezi
Siri ya nyota, siri ya angani
Siri ya njozi usingizi
Siri ya kitandani
Ila siri ya penzi, siri ya moyo
Siri ya nani?
Siri ya chozi ni maumivu ndani kwa ndani
Mapenzi niliyaanzisha yakanifurahisha
Yakanibadilisha jamani
Na sio tu kumridhisha
Nikamdhaminisha, nikamtamulisha nyumbani
Sasa leo yamekwisha yananidhalilisha
Yananiaibisha hadharani
Ila yote ni maisha, japo nahuzunika
Eeh wa kuninyamazisha ni nani?
Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini
Kasuku ndege wangu leo umekuwa bundi
Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini?
Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi
Ile siku unafungasha mabegi
Ulidondosha picha yako dondo
Ndo naypjilazia kwa bedi
Aki ya Mungu umenipiga zongo
Naomba msalimie shemeji
Aki ya nani amepata chombo
Na kama ukiskia nimededi
Jua ni mawazo msongo
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nikiwa na marafiki kwenye sura naongopa
Ila moyo unasota
Nikiwa peke yangu siwezi
Chozi linanidondoka
Nahisi kama naota
Hivi kweli umeondoka
Yanautesa moyo mapenzi
Mpaka kupenda naogopa
Umesema hutaki tena kuiona sura yangu
Kwenye simu umefuta namba zangu
Ila jibu lipo kwa Mola wangu
Mi nasubiri
Kila baya unasema ukitaja jina langu
Umesahau yote mazuri yangu
Basi nilindie madhaifu yangu
Unisitiri
Sijuti kukufahamu, ila najuta kukuamini
Kasuku ndege wangu leo umekuwa bundi
Pokea zangu salamu, bado sijui nitapona lini?
Umevunja moyo yangu, we ndo ulikuwa gundi
Ile siku unafungasha mabegi
Ulidondosha picha yako dondo
Ndo naypjilazia kwa bedi
Aki ya Mungu umenipiga zongo
Naomba msalimie shemeji
Aki ya nani amepata chombo
Na kama ukiskia nimededi
Jua ni mawazo msongo
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
Nenda, salama nenda
(Nenda salama, oooh)
Mwenzako naogopa, ogopa iyeaaaaah
Kila baya unasema ukitaja jina langu
Umesahau yote mazuri yangu
Basi nilindie madhaifu yangu
Unisitiri
(Kamix Lizer)
Ecouter
A Propos de "Nenda "
Plus de lyrics de l'album My Voice
Plus de Lyrics de MACVOICE
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl