JOH MAKINI Content cover image

Paroles de Content

Paroles de Content Par JOH MAKINI

(Bobo made it)

Content(Maudhui)
Content eeey

Content, content, content, content
Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)
Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)

Pambana hela yote tuvunje manyozi(Content)
Nukisha kivyovyote tugonge maviews(Content)
Ubora umeadimika shinda bikra, excellence is missing
Ni kama zima jalalani fikra, takataka discipline
Masela hawagongi like picha mpaka waone Gstring
Brand zinawekwa rihani, mambo ya ndani hadharani
Ni funza wamejaa vichwani ama ni kutafta kukaa hewani
Chap chap utambi yaani, umaarufu ni pombe gani?

Matap tap kabisa yaani
Kuna kufunga ndoa, kutafuta familia na watoto wa kulea
Na kuna kufunga ndoa kutafuta content, mambo ya kuongelewa(Content)
Kulia lia kwenye interviews, kuchafulia majina ma ex(Content)
Kupagawishwa na kubreak manews, kujichulia vifo kiwepesi(Content)

Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)
Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)

Tunapenda sana ichukue nafasi yake (Content)
Tunataka ukweli ukalie kiti chake(Content)
Tunapenda sana ichukue nafasi yake (Content)
Tunataka ukweli ukalie kiti chake(Content)

Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)
Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)

Wanasema wasanii elimisheni(Content)
Mara ooh wasanii badilikeni(Content)
Wakiskia kuna video chafu ambayo imesambaa
Hawana haya kutafuta maconnection
Wanasaka maconnection 
Kumbe kuna jinga lipo kwenye mission
Kuna jinga linatafuta ma attention
Attention please

Usinimind mwana take it easy
Kuna kazi nataka kurelease
And I know yule wali ndizi(Content)

Mahubiri siku hizi si ju ya nini Adamu alikula tunda(Content)
Mahubiri siku hizi ni juu ya habari ya kula tunda(Content)
Wanasiasa wanatengeneza brand hawazingatii maendeleo(Content)
Wanazingatia picha na wanakijiji kuliko maendeleo ya kijiji(Content)
Cha msingi kule kwenye mitandao ionekane ameondoka na wanakijiji(Content)

Msanii mchanga unaumia na sio kweli kwamba hujui mziki
Jamaa wanasema huzungumziki, huna matukio interview vipi?(Content)
Hatununui pombe kupandisha kwa kichwa
Tunasaka mapicha kupandisha kwa Insta
Vile tukishindwa kujikomboa Africa
Tunajikuta tu ulaya mababy sitter
Maumbea maudaku tuko Insta 
Harakati si tunazifanya twitter

Tunapenda sana ichukue nafasi yake (Content)
Tunataka ukweli ukalie kiti chake(Content)
Tunapenda sana ichukue nafasi yake (Content)
Tunataka ukweli ukalie kiti chake(Content)

Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)
Maudhui maudhui maudhui, maudhui, maudhui(Content)

Ecouter

A Propos de "Content"

Album : Content (Single)
Année de Sortie : 2020
Copyright : (c) 2020
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Feb 14 , 2020

Plus de Lyrics de JOH MAKINI

JOH MAKINI
JOH MAKINI
JOH MAKINI
JOH MAKINI

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant

A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl