FID Q Siri ya Mchezo cover image

Paroles de Siri ya Mchezo

Paroles de Siri ya Mchezo Par FID Q


Nilipotoka mbali na naheshimu nilipo
Sikuona umuhimu Kivu Steves kanipa elimu ya Biko
Kimaandiko, kimistari mafans wanascream kirap
Sikuamini kama nina rally, mpaka ilipo bin heba

Wanapagawa, na baadhi ya mambo ninayo yajua
Pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua
Wapagawa, na nipo mgumu wa team Beatles
Achana na power windows, sijui rims za dimpoz

I let you pimp mshiko, stylish simple
Sanaa iko hivyo sometimes hukaata kukaa ulipo
Wanaodharau juu tu yaletea matatizo
Hawajui kama dau pendelea kukuona hivyo

Bonge la style, mbonge la njaa hauna kitu
Jikombe ugongwe ili mtaa wakuone hauna issue
Ukishindwa kujiandaa, jiandae kushindwa
Mjinga utaachwa unashangaa, kumuona Martin kadinda

Usmachi anaotinga, majumba madinga
Ya bwana Almasi juu hizi traki za harakati ni ujinga
Hapana, nguvu ya mamba ni maki
Na umaarufu haukutamba, kushika namba ni basi

Sio kipaji ka bande tu, tunachana kiguu
Kisa traki ikivuma sana kwenye chati duu
Amani kwa Chachage, na makwado sio kulia
Baba asante kwa utafiti na zaidi ya almasi bandia

Nyumbani, nasikiliza dunia ya Sasa Marijani 
Najiuliza utaridhi nini?
Ikiwa imani ishakwisha tangu zamani
Labda kubisha na akitisha na jani
Inasikitisha unapojua na aliyekupigisha ni jirani

Pole Mapusoo ni uchumi umefanya umetubu
Wazee wahuni hadi so way back before sugu
Taifa la kondoo, bondeshwa na serikali ya dubu
Na mbwa mwitu mwenye siri, ili bepari umwabudu
Kimahakama, kiserekali kidini umsujudu
Huo ni uchumi wa pia, unafanya vijana wanaumia
Tunaishia, kufia mabatani kama nzi ndani ya glasi ya bia
(Bia, bia, bia.....)

Siri ya mtungi aijuae kata, komaa kaza kisha utapata
Siri ya mtungi aijuae kata, komaa kaza kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tuu, na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi tuu, na hakuna mwingine

Tofauti ya biashara na siasa 
Kila hasara inaeza vuma 
Wakati siasa kila mara
Ukiwa na nara ujue kuna kinara
Anayeunda msafara wa wanaojituma
Na kuchuma kwa kufanya 
Uwe imara kwa fala hakuna

Kidumu chama cha masela(Kidumu)
Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera
Tuone kufuru zaini ya hela 
Tanzania ni dem wa mtungu, wanamuita 'cha wote'
Hangover, anayekimbia kwa kupiga mtungi saa zote

Kubwa anazuga ata solve, matatizo nchi yake
Na gari bovu halisukumwi kwa kukaa ndani yake
Maendeleo ni ile ndoto, mwekezaji ashaepuka
Ju ya kukaa karibu na moto, ni kuota kujiunguza

Na hakuna uhuru wa kweli, msidanganywe na elusion
Na daily tunafeli, sababu ya political institution
Civilization in my advance, sasa wanatuua economically
Na hakuna uchumi mbaya kama ule wa kujiona huko free

Kusaka ukweli saa kumenya kitunguu
Kila ganda utatoa machozi na utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua
Zaidi ya mafela yaliounganika 
Je utayaghairi ukiyafunua?

Wamejivisha U-Noah, sarafina zao zikatoboka
Wakajivisha U-Musa, fimbo zao hazikugeuka nyoka
Sasa unaujaribu Mungu mtu, kuamua nani leo atatoka?

Siri ya mtungi aijuae kata, komaa kaza kisha utapata
Siri ya mtungi aijuae kata, komaa kaza kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tuu, na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi tuu, na hakuna mwingine

Ecouter

A Propos de "Siri ya Mchezo"

Album : Siri ya Mchezo (Single)
Année de Sortie : 2019
Copyright : (c) 2019
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Aug 24 , 2019

Plus de Lyrics de FID Q

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl