Paroles de Intro
Paroles de Intro Par DOGO JANJA
Kwa jina naitwa Zaituni Omari Salim
Mamake mzazi na Abdulaaziz Chande almaarufu kama Dogo Njanja
Mwanangu alianza kuimba akiwa na umri mdogo sana
Ila sikudhani kama angefika hapo alipo
Alipokuwa anaimba kidogo kidogo anachukua madaftari anaandika
Mi najua ni mambo ya shuleni nikimuuliza ni nini anasema ni mistari
Kwa hio nikawa namgombeza kazana kwanza na masomo
Achana na mambo ya mistari
Ukifikia umri uta...nani tu, utafanya hio kazi yako
Baadae kweli mi nikawa nachukulia mzaha
Ivo ivo anaendelea kuimba
Ikiwa kuna mashindano ya nane nane akatoka
Alipoenda kuimba huko kwenye nane nane mi sina taarifa
Majirani wakaniambia fungulia redio msikilize mwanao anaimba
Nilipofungulia redio kweli nikakuta ni yeye anaimba
Basi nikawa nasubiria tu aje...
Alipokuja akaniambia 'mama nimeimba kwenye nane nane nimeshinda'
Nilishiriki mashindano kwa iyo nimepata ushindi
Nimepewa ofa ya kwenda kurekodi
Basi watu wakanishauri kwamba wewe
Usimkataze mwache aendeleze kipaji chake
Hapo atakapomaliza elimu ataendelea
Kwa hio alikuwa anapenda sana mziki tangu udogo
Sasa alipokuwa shuleni akapata hio ofa ya kwenda kurekodi karekodi
Akafanikiwa kweli....akawa anafuata wasanii wakubwa kama;
Akina Madee na Madee kweli alimsaidia
Namshukuru sana Madee kwa sababu alimsaidia na--
Na bila hivyo sababu hapa Arusha watoto wanaharibika sana
Lakini Madee aliona kipaji chake alikigundua
Na akamchukua akamsaidia, kwa iyo namshukuru sana uongozi wake
Nasema Asante Mungu kwa Anko kuwa mpaka saa hivi alipo
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa mwanangu kipaji
Na kuwa yeye ndo tegemeo katika familia
Namwombea Mungu sana amlinde na ambariki
Nasema ASANTE MUNGU...ASANTE
Ecouter
A Propos de "Intro"
Plus de lyrics de l'album Asante Mama
Plus de Lyrics de DOGO JANJA
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl