Unikumbuke Lyrics
Unikumbuke Lyrics by FELIX OMENDO
Siri ya msalabani ina Mungu mwenyewe mikononi mwake
Yesu aliposulubiwa na wezi wawili kando kando yake
Wa kwanza akasema kama wewe ni Mungu, jiokoe pamoja nasi
Mwingine akasema inapasa kuhukumiwa
Makosa ni yangu ila bwana amekosa nini
Bure amesulubiwa sababu ya matendo ya dhambi
Ili Kwa jina lake niokolewe eeh
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe Yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe Yesu uniokoe
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe Yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe Yesu uniokoe
Hili ni ombi langu mchana na usiku bwana
Nipate neema na kibali makosa yangu uniondolee
Cha kukulipa sina, wewe ni wa dhamana
Mimi bado nakaza mwendo nifike kule uliko nitengea
Kwa sababu ya dhambi na makosa yangu ulivuliwa kanzu.
Ukawekwa msalabani ili macho ya watu wote yashuhudie
Uliyekomboa Unayekomboa Utakayekomboa ni wewe Yesu
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe yesu uniokoe
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe yesu uniokoe
Nipate mwingine wapi anayependa kama wewe
Uliyenipenda kwanza kabla hata mimi nikujue
Tena Sheria zako umeziweka moyoni mwangu
Na bado unanichunga katika njia zako nisipotee
Mwokozi wangu unirehemu kwa nyakati zote
Moyo wangu unatamani nisiangaike na mambo mengine
Wokovu wangu ninauweka mikononi mwako
Kila siku uniongoze bwana yesu
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe Yesu uniokoe wa dunia
Ewe Yesu uniokoe
Bwana Yesu unikumbuke
Uwapo paradiso usinisahau
Haya ni makosa yalonipasa
Lakini ewe yesu ulibeba yote
Wewe ndiwe mwokozi wa dunia
Ewe Yesu uniokoe wa dunia
Ewe Yesu uniokoe
Watch Video
About Unikumbuke
More FELIX OMENDO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl