Almasi Lyrics by DIZASTA VINA


Nilikutana mtaani na Mzee mmoja
Tukaketi chini akanipa soga
Mimi sitamsahau
Alisema wangapi walikuwepo namba moja
Sasa wamerudi chini ni vioja
Watu wamewasahau

Utavamia kwenye tamasha la muziki
Usoni bashasha huku rohoni umeikumbata dhiki
Sanaa imesanda na sasa tena hauna kiki
Utaigiza furaha kwa kunywa bia za mashabiki
Zitaongea nguo ulizoazima kwa msela
Hazitatosha kuficha ukweli kwamba hauna hela
Hautakumbukwa kama mwanzo wakati unatisha
Paparazi hawatakujua so hautapigwa hata picha
Hakuna atakayekuangalia usoni
Tamasha utaingia kwa kuzidandia kuponi
Mchumba uliyemmwaga atang'ang'aniwa kiunoni
Utatabasamu huku hasira umeifungia moyoni
Utapotaka kujichanganya utahisi haya
Lipsi denda zitachakaa kusizi kaya
Watasikika wadadisi wakiongea kwa kudisi
Kamera zote zitamfata msanii uliyemu-Inspire
Hayatakuwepo majumba magari na mapochi nene
Milo ya hoteli za kifahari na ma-roast kede
Zitasahaulika idadi ya tuzo ulizohodhi kwenye majukwaa
Huku magazeti yakiku-Post mbele
Hautatembeza tena rungu ka' Kipepe
Hautavutia Wachuchu maana nyota haina nguvu
Hautafatwa tena na Mashushushu kwa maseke
Utakumbuka ulivyozungukwa na grupu la Vicheche
Michuzi itakauka utapiga hodi ukame
Hautawekwa kwenye ma-board ka' Van Dame
Hautashawishi magari road yapangane
Na utakuwa peke yako bila ya ma-Bodyguard nane
Kipindi ambacho taswira yako ipo gado
Ndo' kipindi cha kulikata shauri lako
Kutambua nafasi na thamani ya sauti yako
Kutambua dhamana mapema kabla ya mauti yako
Dhamana yako ni zaidi ya kula na  kupiga pamba kali
Kununua Bupa na chupa ukizilaza chali
Jina kubwa likikufumba ushindwe tafakari
Utakufa masikini ukizubaa kuzichanga mali
Usijesahau maisha yako halisi
Yanayolingana na kipato chako thabiti
Usijekufa kipindi ambacho michango haikidhi
Haitoshi hata kujenga nyumba ya mama'ako Kibiti
Uko wakati wa kumiliki idhini ya uwongo wako
Wenzako wamedondoka, Je utajifunza?
Unasifika mjini kwa wingi wa longo zako
Ukifa tutasimulia nini watoto wako
Tutasimulia idadi totoz ulizonusa
Au gambe idadi ya Kopo ulizoruka
Idadi ya mahusiano au idadi ya mioyo uliyoivunja
Au idadi ya wasichana wadogo uliowavuruga
Najua mwisho mwanangu hamna njia
Utatokewa na kila hadithi uliyoisikia
Sicho kitu ninachokihofia
Hofu yangu kama umeshaiandaa saikolojia
Ukija wakati pazia halifunguki
Wadananda uliowadandia hawakukumbuki
Najua itafanya akili ichoke utapagawa
tafadhali usijegeukia pombe na madawa
Kipandacho hushuka ulishawaza
Si muiujiza ni asili inayoshangaza
Wasahaulifu Walimwengu ilitangazwa
Watataja mashujaa na jina lako halitatajwa
Wanafki, Walafi na Mabishoo zako
Wangapi watakuwepo kiu ikidaka koo lako
Muda wa kuwasoma wote waliopo kando yako
Maana hata pesa haitatibu jelaha la roho yako
Maagano ya siri yatakuwinda
Vyote walivyotabiri vitafika
Maisha ya ndoto yataisha
Utairudia kawaida utagundua kuwa haukuwa malaika
Kiasi utajua dini
Utajua harufu ya sakafu kwa maana utakuwa chini
Hata maana ya maisha itapotea
Sumu, Kisu na vitanzi vitasogea
Sikutishi ila utakufa peke yako
Jeneza lako halitabebwa na hao vicheche wako
Sishangai wenge lako, Ng'ombe
Nashangaa unapoyumba kwa kuzidiwa na ukubwa wa pembe lako
Ni heri kuwa mwewe
maana mwoga anajali kuwa uelewe
Kundi la watoto nyumba wanakupenda
Na wanaota siku moja waje kuwa kama wewe

Watch Video

About Almasi

Album : The Verteller (Album)
Release Year : 2023
Added By : Farida
Published : Jun 17 , 2023

More DIZASTA VINA Lyrics

DIZASTA VINA
DIZASTA VINA
DIZASTA VINA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl