Teta Nao Lyrics
Teta Nao Lyrics by CHRISTINA SHUSHO
Ee Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami
Ee Bwana utete nao wanaoteta nami
Upigane nao wanaopigana nami
Uishike ngao na kigao usimame unisaidie
Uutoe mkuki uwapige ooh wanaonifuatia
Uwaambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako
Uutoe mkuki uwapige ooh wanaonifuatia
Uwaambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako
Wananiuliza mambo nisiyoyajua
Ee bwana utete nao wanaoteta nami (Bwana pigana nao)
Upigane nao(pigana nao)
Wanaopigana nami (naomba wee nitetee)
Ee bwana utete nao (nitetee)
Wanaoteta nami(Baba nitetee)
Upigane nao (pigana nao)wanaopigana nami
Waaibishwe, wafedheheshwe
Warudishwe nyuma wanaotafuta nafsi yangu
Wafadhaishwe, wawe kama makapi
Mbele ya upepo
Malaika wa bwana waangushe chini
Wananilipa mabaya, badala ya mema
Kutwa kucha waniwinda, ili niteseke
Kiganjani mwako niweke (ee Mungu wangu)
Ubavuni mwako nikumbatie (Jehova wangu)
Mikononi mwako uniweke (ee Mungu wangu)
Ubafuni mwako nikumbatie (Jehova wangu)
Eehh
Ee bwana utete nao wanaoteta nami (Bwana pigana nao)
Upigane nao(pigana nao)
Wanaopigana nami (naomba wee nitetee)
Ee bwana utete nao (nitetee)
Wanaoteta nami(Baba nitetee)
Upigane nao (pigana nao)wanaopigana nami
Njia yao iwe giza na utelezi
Malaika wa Bwana, akiwafuatia
Uharibifu wapate kwa ghafla
Waharibifu waanguke ndani yake
Mimi bure wasinisimange, bure wasinigonge
Na wovu wao aloficha wamnase mwenyewe,
Ila sababu wamenichimbia shimo la hasira
Mifupa yangu, wataitazama, Bwana ni nani
Aliye kama wewe na nafsi yangu, itamfurahia Bwana
Wapendeza Bwana wapendeza, ee Bwana wapendeza
Katika hili najua utatenda aah
Nitetee Bwana nitetee, ee bwana nitetee
Katika hili najua utatenda aah
Wapendeza Bwana wapendeza, ee Bwana wapendeza
Katika hili najua utatenda aah
Nitetee Bwana nitetee, ee bwana nitetee
Katika hili najua utatenda aah
Wapendeza Bwana wapendeza, ee Bwana wapendeza
Katika hili najua utatenda aah
Nitetee Bwana nitetee, ee bwana nitetee
Katika hili najua utatenda aah
Watch Video
About Teta Nao
More CHRISTINA SHUSHO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl