Hila Zimevunjwa Lyrics
Hila Zimevunjwa Lyrics by BERNARD MUKASA
Mungu alipopanga ukombozi
Kusudi kutuosha dhambi hizi
Akakubali kwamba ye'mwenyezi
Afe kifo kibaya kionezi
Mti wakamuwamba kama mwizi
Wakidhani ya kwamba ameshindwa
Amefufuka Bwana na mwokozi
Kazivunja hila za Lusiferi
Katukomboa wana wa mwenyezi
Twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri
Mungu akakubali kuonewa
Hakuweka wakili kutetewa
Nguo bila hiari kavuliwa
Kapigwa misumari kazomewa
Akabaki kusali kuombea
Wauaji wapate msamaha
Amefufuka Bwana na mwokozi
Kazivunja hila za Lusiferi
Katukomboa wana wa mwenyezi
Twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri
Mungu atufundisha kujitoa
Ya wengi maisha kuokoa
Na anatukumbusha kupokea
Yanayotutisha kumwendea
Tusije kukatisha njema nia
Ili kuyapisha ya dunia
Amefufuka Bwana na mwokozi
Kazivunja hila za Lusiferi
Katukomboa wana wa mwenyezi
Twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri
Watch Video
About Hila Zimevunjwa
More BERNARD MUKASA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl