Chama la Wana Lyrics
Chama la Wana Lyrics by BANDO
Mnyamwezi nimeshanyuka pamba
Sembuse kuwanyuka nyie watoto
Madem, vicheche mnaozunguka juu ya moto
Bila hela ni vichomi
Dem wako akilala na dera
Jua kuna mtu anaenda kuchambua ndotoni
Mapenzi ya siku hizi kama hiari
Wengi tunaishi tegeta nyuki
Ila hatujui utamu wa asali
Watacho kwambia we usijali
Maana huwezi kutumia kamba ya rubber
Kukazia buti gari
Wa Makonde ndo anashabikia danda
Unaezakuta mkude simba anae anashabikia Yanga
Wanaposema mi ni mkali nazidisha gundu
Mwislamu ana swali ila anahisi jibu analo Mungu
Oh my God!Kasali vipi usawa unabana
Naliskia eti mchungaji amekula kondoo wa bwana
Yaani noma sana, dunia Dar, ulimwengu shujaa
Ushai jiuliza hivi kipofu naye anaona kinyaa?
Sioni ajabu, mshamba akinyoa denge
Ni ajabu sana kuona hadi mamba kaingia mkenge
Hali ngumu kila sehemu
Ila pesa ndo bwana pekee ambaye anadumu na kila dem
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Aah mamlaka ya hali ya hewa inanisaka na rabii
Eti nachafua anga, navyotema hizi fasihi
Navyo saga hizi laini utasema nina ubongo wa blader
Seremala, yule chonga kitu moto mnachopenda
Kifupi sili chungwa na maganda
Dem wangu guitar maana dem amesave kinanda
Hii serikali ya viwanda, inanipa ndoto mbevu
Nyumbani nimeshajenga banda, nina dream ya kufunga ndevu
Siwezi lala na njaa, nitalala na wife
Ukiona nimeshika kitanzi, ujue nalala na life
Akili ni nywele nachokiwaza kiko mbali
Bonya kipilipili ndo ana akili ya kachumbari
Ah mziki wito wengi wanachana ila hawana sifa
Mchezo simple dana dana ila hauhitaji keeper
Utani mwiko, nilipo hauwezi figure
Unaweza ukawa fundi jiko na bado usijuwe kupika
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Ah, na mapigo ya kila style tae kwon ndo mpaka kung fu
Hadi -- naipakia buturu
Sasa twanga ukoboe usikodoe
Naposema akili nywele, niambie ni za wapi ili nizinyoe
Am sorry brother, maisha safari isiyo na traffiki
Wanaofika kileleni, gari wanapandiaga wapi?
Sepeni vya ndenzo, mi ni yule Ustadh Bishoo
Mpaka kanzu naivalia mlegezo
Asiye nijua, mwambieni mi ni hatari kwake
Tena hatari sana, shubiri mkewe ni asali kwake
Dem wako ana habari zake?
Ndo yule jamaa mlafi ambaye anakula chakula na mpishi wake
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Dusco dusco bado nyie hamjui kurap mnazuga
Dusco dusco bado mi ndo yule champion kila muda
Mi ni chama la wana, hawajui kama chama la wana
Mi ni chama la wana, hawajui mi ni chama la wana
Watch Video
About Chama la Wana
More BANDO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl