Ujitume Lyrics
Ujitume Lyrics by ALLY MAHABA
(ATL Music beiby)
(S.H.I.R.K.O Shirko media)
Mume wangu kama leo
Huendi kibaruani tuonge
Mi na wewe tuyaweke sawa
Mambo yetu yaende
Unasemaje baby? Umenisikia
Kwanza kaniletee begi, za wapi tena
Nataka niwahi kule
Usije kanichelewesha bure bure
Kutoka kwako ni alfajiri(Umelewa)
Kurudi usiku siri siri(Umechelewa)
Humu tunaishi wawili
Ama unaishi pekee yako
Haya nakaa chini
Unachomaanisha ndio nataka, nielewe
Mi najuwa unataka tugombane umenichoka
Yaani wewe
Huku ulipo wewe mimi sipo
Tumeelewana
Kutwa madeni na huishi mikopo
Mwanamume
Inatosha, inatosha inatosha
(Usiseme hivyo)
Inatosha, inatosha inatosha
(Usinifanye hivyo)
Nataka ujitume(Nitajituma)
Wewe ndo mume(Sawa mama)
Maisha yasigume
Bume ndio nitakuelewa
Kuipata kazi sio rahisi mke wangu
Maisha yapo kama ngazi
Kuipanda mpaka atake Mungu(Naelewa)
Kweli huwezi kupata chochote
Mpaka akupatie Mungu
Bila juhudi zako je we utalipataje fungu?
Unaniona mi kuwa sipendi kazi(Sio kweli)
Mimi ndio kichwa cha familia
Kuhangaika popote mi niko radhi(Nisifeli)
Baby nitapata vumilia
Si uende
Uarabuni ukajaribu bahati yako mwenzangu
Mazonge
Ya viziuzi ubishi wako waovunja moyo wangu
Huko hakuna lolote
Pamoja na mihangaiko yao yote(Ndio maana)
Na ujanja wao wote
Pesa wanazimaliza madem zote(Hapana)
Basi kaa wewe nyumbani
Nami nitoke nikahangaike
Mwanamume unapenda ushindani
Nami nifanyeje mtoto wa kike?
Inatosha, inatosha inatosha
(Usiseme hivyo)
Inatosha, inatosha inatosha
(Usinifanye hivyo)
Nataka ujitume(Nitajituma)
Wewe ndo mume(Sawa mama)
Maisha yasigume
Bume ndio nitakuelewa
Inatosha, inatosha inatosha
(Usiseme hivyo)
Inatosha, inatosha inatosha
(Usinifanye hivyo)
Nataka ujitume(Nitajituma)
Wewe ndo mume(Sawa mama)
Maisha yasigume
Bume ndio nitakuelewa
Watch Video
About Ujitume
More ALLY MAHABA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl