Yuko Mungu Lyrics

ALICE KIMANZI Feat PAUL CLEMENT Kenya | Gospel,

Yuko Mungu Lyrics


Mungu anaweza kufanya njia njagwani
Na mito ya maji nyikani
Kama alifanya masika na kiangazi
Anaweza kubadii majira pia na nyakati

Giza totoro yanizingira
Miale haijanifikia
Ilhali kumekucha, pambazuka
Imani, yashuka yadidimia
Amani nayo yafifia
Eloi lama sabachthani

Yuko Mungu anayeweza
Yuko Mungu anayetenda
Mwamini Yeye, mwamini Yeye
Hutoaibika

Giza likiwa ni zito Bwana atawasha taa
Sababu Yeye ni Mungu mwenye amandla
Atarejesha amani, atarejesha furaha
Ulivyo vipoteza kwa muda mrefu atarejesha mara...

Pale ninaposhindwa nani wakuni wezesha
(Mungu Pekee, ndiye awezaye)
Na nikiwa vitani nani wakunishindia
(Mungu Pekee, ndiye awezaye)
Napokuwa mdhaifu, nani wakunipa nguvu
(Mungu Pekee, ndiye awezaye)
Ninapotia shaka, nani wakuniongoza
(Mungu Pekee, ndiye awezaye)

Yuko Mungu, Mungu yuko....

Leave a Comment