Corona Lyrics by ZANZIBAR ALL STAR


(Zanzibar All star iyee)

Huzuni imetawala dunia nzima
Corona
E Mola tulinde tupate uzima 
Na Corona

Jilinde, linda na familia yako
Ianze kwako na rafiki zako
Epuka mzaha na mikusanyiko
Isiyo na maana

Jilinde linda na familia yako
Ianze kwako na rafiki zako
Epuka mzaha na mikusanyiko
Iso na maana

Tusimame kwa pamoja...
[John Pombe Magufuli]
Imetokea hatari
Corona corona corona inaua 
Corona corona corona ni hatari corona

[Chaby Six]
Rais wetu Tanzania
Hii ni homa ya dunia
Mungu simama kama ngao 
Na tiba kututibia

Mola ponya Tanzania
Na haya maradhi ya sasa
Tulinde na corona
Hata na ukimwi na Cancer

Mungu ibariki Italia
China Uingereza 
Weka ngao kwa Tanzania
Marekani na Iran
Na nchi zote za dunia

[Zenji Buoy]
Naona dunia ina machozi 
Na watu ndio waliyao
Sio wananchi tu hadi wananchi wameguswa usisahau
Zingatia maagizo ya wizara ya Afya
Kujikinga na kiwiko cha mkono ukipiga chafya
Anko tumia kitamba ukiwa na kikohozi ghafla
Jiepushe na maambukizi kwa ajili yako na Taifa

[Sultan King]
Mungu Baba tuepushe na Corona
Yeiyei yeaah aah
Ee Mola tunusuru waja wako
Na hili gonjwa baya Corona
Hakuna kimbilio zaidi ya kwako
Na wewe ndiwe dawa ya kuponya

Ee Mola tunusuru waja wako
Kwa hili gonjwa baya Corona
Hakuna kimbilio zaidi ya kwako
Na wewe ndiwe dawa ya kuponya

[Yoram]
Ooh, oooh... ziba mdomo unapopiga chafya au kukohoa
Ooh, oooh... nawa mikono yako kwa maji yanayotiririka
Ooh, oooh... epuka mikusanyiko isiyo ya lazima
Ooh, oooh... unapohisi dalili za homa ya Corona 
Nenda kituo cha afya

[Rico Single]
Okay osha mikono yako kwa maji ya kutiririka
Tena mara kwa mara kwa sabuni na uhakika
Epuka kupeana mikono wakati wa kusalimiana
Epuka mikusanyiko tujihadhari eey

[Sapina]
Ee Mola nusuru dunia yangu
Vizazi pamoja na nchi yangu
Corona si rafiki yangu
Adui wa uhai wangu

[Pozza]
Fellow Tanzania inabidi tuwe care
Vyanzo vyetu vya uchumi wengi kwenye mkusanyiko
Ndio tunapata mshiko
Baas ndugu na jamaa mniskize mi
Ukiwa na homa na mafua usipuuzie kabisa
Kichwa kukuuma na mwili kukosa nguvu
Ni moja ya dalili

[Smile]
Jikinge dhidi ya homa ya Corona
Corona

[Sultan King]
Ee Mola tunusuru waja wako
Na hili gonjwa baya Corona
Hakuna kimbilio zaidi ya kwako
Na wewe ndiwe dawa ya kuponya

Ee Mola tunusuru waja wako
Kwa hili gonjwa baya Corona
Hakuna kimbilio zaidi ya kwako
Na wewe ndiwe dawa ya kuponya

[Yoram]
Ooh, oooh... ziba mdomo unapopiga chafya au kukohoa
Ooh, oooh... nawa mikono yako kwa maji yanayotiririka
Ooh, oooh... epuka mikusanyiko isiyo ya lazima
Ooh, oooh... unapohisi dalili za homa ya Corona 
Nenda kituo cha afya
Kinga ni bora kuliko tiba

Ukiwa na dalili piga hizi namba bure
Itakusaidia  0800110037 eeh mama eeh
Ama 0800110124

[Laki]
Epuka taarifa za uwongo
Wananchi wote fuata maelekezo

Corona, Corona ee Corona inaua
Usilete masihara
Corona sio mchezo

Watch Video


About Corona

Album : Corona (Album)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : May 01 , 2020

More ZANZIBAR ALL STAR Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2023, We Tell Africa Group Sarl