Ni Wewe Worship Medley Lyrics
Ni Wewe Worship Medley Lyrics by SYLVIA AKOTH
Mungu wangu ni wewe, Jehovah ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Mwenye enzi yote na utukufu ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Mwenye nguvu zote, heshima yote ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Mwenye enzi yote nakuinulia macho yangu
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Eeh baba niseme nini mbele zako
Wema wako niulinganishe na nini bwana
Umekuwa kimbilio maishani mwangu
Umekuwa tegemeo maishani mwangu
Mali niliyo nayo ni juu ya neema yako
Umbali nimefika ni juu ya neema yako
Ingekuwa mwanadamu singestahili lolote
Ingekuwa mwanadamu singepata chochote
Ni juu yako tuu niko jinsi nilivyo
Ni juu yako tu niko hapa leo
Eeh Yesu we Yesu we, nani kama wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Alpha na Omega aliyekuwa, atakayekuwa ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Ulinipenda ukaniokoa kwa damu yako
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Kila goti lipigwe, kila ulimi ukiri ni weewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Yesu ni wewe, Baba ni wewe
Uliyeniiita na kunikomboa ni wewe
Uliyeniiita na kunikomboa ni wewe
Niseme nini mbele zako bwana wangu
Wewe ndiwe utaoye katikati ya mavumbi
Tena ni wewe uniketishaye na wakuu
Ni wewe Mungu wangu ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Dawa ya miguu yangu baba ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Uliyenihesabia haki baba ni wewe, ni wewe baba
(Ni wewe Bwana ni wewe, ni wewe Bwana)
Sitambui mwingine sijui mwingine, baba ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Wokovu wangu uzima wangu baba ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Nisipo, kimbilia wewe ni nani mwingine
Nisipo, mtazamia wewe ni nani mwingine
Vizazi hata vizazi vyakufamu wewe
Dunia yote yakufahamu wewe
Ni wewe (Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Kimbilio langu mwamba wangu ni wewe
Baba ni wewe (Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Mungu wa majira yote
Hakuna likushindalo kamwe
(Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Uliye na haki ya uzima ni wewe, ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Mungu wa milele, Mungu wa ushindi ni wewe
(Ni wewe Bwana ni wewe Bwana)
Ni wewe ni wewe Yahweh
Dunia yote iko mabegani mwako
Wewe ni nguvu yangu Yesu
Umeinuliwa juu
Ufalme wako ni wa juu yesu
Umejawa na ukweli na haki
Hakuna kama wewe
Bila wewe Yesu wee, siwezi
Bila uwepo wako, siwezi
Bila nguvu zako kwangu, siwezi
Nimetambua bila wewe, siwezi
Baba bila bila uzima wako mi siwezi
Baba bila kusema nami baba, siwezi
Naamini nitakuwa mgeni wa nani bila, siwezi
Naamini ni nani anayenipenda mimi bwana, siwezi
Hakuna aliye aliye aliye
Hakuna aliye kama wewe Mungu wangu
Hakuna aliye aliye aliye
Hakuna aliye kama wewe Mungu wangu
Hakuna aliyenifia msalabani
Hakuna aliyeniokoa kama wewe
Hakuna aliyelipia gharama
Hakuna aliyenipenda kama wewe
Hakuna aliyee, aliye aliye kama wewe
Kwake Jehovah tumesimama leo
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni Yesu
Kwake Yahweh tumesimama leo
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni Yesu
Kwake Messiah tumesimama leo
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Ndiye mwamba ni Yesu
Aliyeniumba ni yeye Bwana wangu
Ndiye mwamba ni Yesu
Aliyeniita,
Ndiye mwamba ni Yesu
Aliyenikubali ni yeye bwana
Ndiye mwamba ni Yesu
Ndiye mwamba, ndiye mwamba
Ndiye mwamba ni Yesu
Ndiye mwamba, ndiye mwamba
Ndiye mwamba ni Yesu
Ndiye mwamba, ndiye mwamba
Ndiye mwamba ni Yesu
Ndiye mwamba, ndiye mwamba
Ndiye mwamba ni Yesu
Watch Video
About Ni Wewe Worship Medley
More SYLVIA AKOTH Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl