Utata Lyrics
Utata Lyrics by SUSUMILA
+254, 001
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Bila pesa mapenzi shida
Mpenzi anaona mnapoteza mida
Utampa kipi umechacha
Yeah akita doh unampa ratiba
Unatamani uwe mwizi uende kuiba
Hata umpende vipi atakuacha
Yeah wanasema elimu ni ufunguo wa maisha
Eti ndio mtaji
Vipi tuso na pesa za kwenda chuo tumekwisha
Na tuna vipaji
Peace, kwa brother Joho 001
Peace, mi nakuita King Sultan
Peace, kijana wako niko vitani
Peace, napambana mkono uende kinywani
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Tushanuka moshi ghetto matope majiko kuni
Kwa mangi nikope sura napauka na maisha duni
Sijamuona anayetabasamu kila nayemkuta ni huzuni
Karibuni ila ukiondoka jidondoe kuna kunguni
Tunabishana na wasomi tunagongana mabega
Vyeti vinaishia kabati tupate kwa boda boda
Nyumbani mlo mmoja nyingine ya kulipa keja
Usishtuke kwa bega ukiwa soft unaishia uteja ah
Nishaona hadi madada wanaliwa hadi jicho
Kwa kutaka msaada kisa maisha sio simple
Wanapata magonjwa ama kuishia uja uzito
Msongo wa mawazo nishaona mabraza wakishika pistol
Peace, hongera wapambanaji wote
Peace, usikate tamaa siku zote
Peace, amini riziki ni popote
Peace, kuna utata ila usiogope
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Uta utata, uta maisha utata
Yaani mwanangu angejivunia
Mi mwanangu ni msanii
Karo mziki angenilipia
Nionekane kwa TV
Ningeishia kwenye zege mijengo
Niwe seremala ama fundi wa kushona
Leo nimepanda ndege malengo
Na mara kwa mara nyota njema naiona
Peace, kwa brother Joho 001
Peace, mi nakuita King Sultan
Peace, kijana wako niko njiani
Peace, napambana nilete sima nyumbani
Uta utata
Watch Video
About Utata
More SUSUMILA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl