Wajinga Nyinyi (Part 6) Lyrics
Wajinga Nyinyi (Part 6) Lyrics by STORI ZA KAPEDO
Hello mum, I hope uko poa
Mi niko tu bado nang'ang'ana
Si ni wewe unilinifunza nizoee kukula jasho langu
Ju crime si poa
Na mi bado najikaza kisabuni lakini bado siwezi afford soap
Sijui kama umeona kwa news vile watu wanabebwa na maji
Unajua mbona? Ni ju pesa ingetengeneza drainage system
Iliflow kwa mifuko za watu, I mean, ilikunywa maji
Na imekuwa ngumu kupata justice ju ukihire lawyer wananunua judge
Saa hii ukiuliza kesi ya Sharon iliendaje?
Utaskia Ooo-Bado tunafuatilia
By the way mum, after kumaliza shule nilipata kazi
Na ni ya kutafuta kazi
Si unajua ukiwa na kazi siku hizi hiyo si kazi
Kazi ya kutafuta kazi ndio kazi lakini ukiwa na connections sio kazi kupata kazi
Enyewe if education is the key then heri wote tungesomea kuwa key cutter ama fundi wa locks
Ju graduation parties zimejazana maua lakini huku nnje maisha sio bed of roses
Wale wanasema vijanaa tujiajiri wameajiriwa
Mum tuliamka mapema tukapigia hawa politicians kura ndio wapite
Siku hizi kwa traffic ni siren wakituharass ndio wapite
Wapite? Ndio wafike kwa parliament walale
I guess ndio maana wako na pay sleep
Depression imefanya wazazi ndio wanazika watoto
Na cost of living iko high mtu hata hawezi afford kamba ya kujinyonga
Naskia mtoto hajazaliwa ako na deni China
Na kesho headlines zitasema uchumi imepanda
Imepanda? Ni sawa tu Mungu anawaona
Cheki, si ati na dis-respect the dead
Lakini mheshimiwa akikufa na Cancer ni headline
Mwananchi akikufa na Cancer inakuwa statistics tu
Btw mahindi ina aflotoxin iliingiaje kwa port?
Kama sio mtu alipewa za macho ndio afunge macho
Siku hizi hadi siasa inapigwa kwa mazishi
Na wakipatana ni kurushiana maneno na matusi haziishi
Ona wanasubiri sportsmen wakufe ndio wakawacelebrate kama heroes
Ni sawa tu Mungu anawaona
Mum, is it true that mtu akiwa na pesa anaweza nunua justice?
Mbona tunasahau siri ni kama mimba ata uifiche aje itajitokeza
If politicians ndo wasemaji wetu, niambie tuligeuka bubu lini
Si niheri tujifunze sign language tupige kelele nayo
Niambie kama vijana ndio leaders wa tomorrow, kesho ni lini?
Ni ukweli kuna pesa ilipotelea Afya House ndio maana mwananchi hana good health care?
Na mheshimiwa akipata homa anakuwa airlifted na ndege
Huku treatment anapelekwa abroad
Ni ukweli zile wheelbarrow walinunua 100k zilikuwa za kutubeba wana
Ni swali tu, ati bado kuna IDps kwa camp wakati politicians wanagrab mashamba
Ati kuna politician alibebwa na ndege akafungue class imejengwa na matope
Aii mum sio sawa, hawa politicians wanalalia King Size bed
Wakati hospitals zina admit watu wawili kwa kitanda moja
Ni sawa tu Mungu anawaona
(Mum kata simu kwanza wacha niongee na hawa mapoliticians one on one)
Nyinyi mapolitician wakati wa kupiga kuta tulimark tik
Kumbe tunamake wrong choices
Cheki mmegeuka viziwi hata parliament iwe na speaker hamskii
Mlienda sherehe bunge that's why mlitaka tuwachague via political parties
Angalia hatuko mbele pamoja ni kama tulifananisha ndimu na chungwa
Ju speed ya maendeleo kwa ground sio chap chap
Na shuku ni ju tulichoose governor
Siku ya mwizi ni arubaini lakini ya politician ni siku bond imekatika
Human rights ni upande wa kulia, rip Willy Kimani
Whistle blower wamekatiwa pumzi
Msidhani nitachicken out bila kumention ile stori ya chicken
Cheki tunaishi maisha ya hand to mouth ni kama body parts zingine hazina maana
Hivi hii ndo motherland yenu, mbona watoto wenu wanaenda majuu for further studies
Angalia mmetuwachia school motto na baridi ya ujinga inafreeze brain ya watoto
Hata tuchange syllabus, mnatusoma mnaprove sisi ndio silly basi
Wapi hiyo spirit ya Mau Mau if tuko busy tunauma uma mali ya umma
Cheki tunageuka banana republic mahali kuna political party ya chungwa
Kama ni pudding mlitaka si mngesema mapema
Anthem inasema tuwe na plenty within our borders
Wakati mmejaa dream ya kushika passports mkaishi majuu
Na kwa boy wa ghetto, greener pastures ni akina veve tu
Na visa anatambua ni kisa za rape na wizi wa kimabavu
Na kanisa siku hizi zinaongozwa na dad and mums
But hawako willing kufungulia milango street children
Ni sawa tu Mungu anawaona
Watch Video
About Wajinga Nyinyi (Part 6)
More STORI ZA KAPEDO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl