Mapenzi ya Kweli Lyrics
Mapenzi ya Kweli Lyrics by STEPHEN KASOLO
Bwana mwenye mapenzi ya kweli
Penzi ya kweli
Niliodhani watanipa raha
Waliniacha kwa kilio
Nilioona wa karibu sana
Walinipasua moyo
Lakini mimi sifi moyo maaana
Haya Yesu alipitia
Na tamanio langu kubwa mimi
Ni kumuona bwana
Nitamuona Bwana mwenye mapenzi ya kweli
Nitamuona Bwana na kilio kitapona
Nitamuona Bwana anibariki kwa furaha
Na mambo yaliyonivunja moyo yasahaulike kabisa
Mambo mengin tunayopitia yanatuacha kwa maswali
Kwanini mimi nipitie haya na ninampenda Mungu
Lakini mbali twasahau kwamba ni mitihani tunafanya
Na ukishinda majaribu yote mtihani umepita
Nitamuona Bwana mwenye mapenzi ya kweli
Nitamuona Bwana na kilio kitapona
Nitamuona Bwana anibariki kwa furaha
Na mambo yaliyonivunja moyo yasahaulike kabisa
Tunaotenda wema kwa wengine tusichoke kutenda
Wanaopanda kwa machozi eeh watavuna kwa furaha
Ole wao walipao wema kwa kutenda mabaya
Utavuna ulichopanda jiepushe na ghadhabu ya Mungu
Nitamuona Bwana mwenye mapenzi ya kweli
Nitamuona Bwana na kilio kitapona
Nitamuona Bwana anibariki kwa furaha
Na mambo yaliyonivunja moyo yasahaulike kabisa
Nitamuona Bwana(Nitamuona Bwana)
Yeye mwenye mapenzi ya kweli(Nitamuona Bwana)
Nitafutwa machozi niliyolia(Nitamuona Bwana)
Nitamuona Bwana eeh(Nitamuona Bwana)
Wacha kulia mama yangu(Nitamuona Bwana)
Utafutwa machozi uliyolia(Nitamuona Bwana)
Mnaolia nyamazeni kimya(Nitamuona Bwana)
Kilio ni usiku nakwambia(Nitamuona Bwana)
Mapambazuko yaja(Nitamuona Bwana)
Umeumizwa moyo nyamaza(Nitamuona Bwana)
Umeumizwa moyo ndugu nyamaza(Nitamuona Bwana)
Nitamuona Bwana
Watch Video
About Mapenzi ya Kweli
More STEPHEN KASOLO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl