ROSTAM Kijiwe Nongwa cover image

Kijiwe Nongwa Lyrics

Kijiwe Nongwa Lyrics by ROSTAM


Alikuja kama masii tukamchangia sadaka
Tukamwona nabii aliyeshushwa siku ya pasaka
Tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe
Eeh-eh na bado wakamlaza nabii kifo cha mende

Hivi unamkumbuka babu? Babu wa Loliondo
Ah-ah yule mfugaji mwenye bleach la kikogo
Watu wamekufa, watu wamefungwa, watu wamepoteza biashara
Sasa umekaribia uchaguzi amerudi chama tawala

Vipi dada yetu wa Igunga, mmh simwoni udangani
Ah mbona ashapata mchumba sio viben 10 wa zamani
Yule fundi gereji chawa, si kamateka bibiye
Na wamefungua mgahawa, yaani wote mama ntilie

Na kuna dem aliyeachiwa mtoto akaolewa na mtoto
Akaachana na mtoto akabaki anamlea mtoto
Hizi ndoa za mjini bwana, zinasikitisha
Eeh maana hufungiwa chumbani na huvunjikia Insta

So soka la Bongo linakwama wapi? TFF maanake nini
Tanzania Football Failure, ndo nacho jua mimi
Unamfukuzaje Amunike ili udhaifu wenu umvuge
Wakati mlimpeleka mlevi ye akacheze namba ya Mkude?

Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero
Ukuta tunavunja kwa tindo
Wameshapigwa guu wako telo
Na kiki za kikolo
Majita tushapiga kishindo

Hili ni fagio la chuma
Linang'oa visiki
Safisha vichaka kwa moto
Simba kageuka duma
Jangwa halipitiki
Ukitufuata umetoa boko

Marehemu walimsema mnyonyaji, kwani mziki una maziwa?
Sasa Mungu kamhitaji na bado hajafanikiwa
Hivi unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo?
Acha maisha yaendelee, jasiri ameumaliza mwendo

Aliyeokota almasi mchangani alikuwa Miss Tanzania
Na aliyekuja inunua dukani ni Mganda aliyekuwa na nia
Ya dhati la pakato akatokea mara mia 
Akawatumia ila mwamba ni mnyanyasaji wa kijinsia

Sa skiza man hii, vipi shem mama Ivan?
Ah tupo tupo tu ila hatupo ka zamani 
Nawe vipi kwani, mbona wife simuoni nyumbani
Hey chill man, sina majibu deal done

Bungeni daily majanga, viongozi wameishiwa mada
Hivi mbunge wako wa Tanga hoja zake unaziskiaga?
Sa nitazisikiaje? Na ana spika mbovu za wana kijiji
Ila fundi wao anakuja soon kutoka Ubelgiji

Nabii Tito na Dr Shika, tayari wamesahauliwa
Mwenzao Mariamu, biriani anapika anapakuliwa
Bongo bwana, ndo nchi inayosupport sana ujinga
Utashangaa Amber Rutty kala shavu ubalozi wa kinga

Yaliyosemwa yamesemwa
Kazi kwenye mmezoea kutema
Wakitaka tuyajenge tena
Waambie muda sio rafiki mwema
(Yeiye iyee, aah aah iyee)

Kusema kweli hatuchoki
Na kwenda jela hatuogopi
Tutabanana ata kama hapatoshi
Hatupindishi ata kwa dumba

Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero
Ukuta tunavunja kwa tindo
Wameshapigwa guu wako telo
Na kiki za kikolo
Majita tushapiga kishindo

Hili ni fagio la chuma
Linang'oa visiki
Safisha vichaka kwa moto
Simba kageuka duma
Jangwa halipitiki
Ukitufuata we toa boko

Watch Video

About Kijiwe Nongwa

Album : Kijiwe Nongwa (Single)
Release Year : 2019
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
Published : Sep 21 , 2019

More ROSTAM Lyrics

ROSTAM
ROSTAM
ROSTAM

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl