Sijali Lyrics by ROSE NDAUKA


Sijali sijali
Sijali sijali sijali...

Asa kwanini unipige pini nashangaa
Mwanga ulikuwa mwingi vipi basi uzime taa
Siwezi tena nyanyuka nimeduwaa
Nishindwe ni vipi wapi nimejikaa

Yaani wanataka mimi nisifike mbali
Nipate matatizo usiku silali
Nawaambie haya yote majaribu
Nisishindane nayo nitakuja haribu

Ila mimi bado ndo kwanza mi nakazana
Sitaacha milele nitazidi kushindana
Watasema lakini nitazidi kupambana
Kweli binadamu ni watu wa ajabu sana

Imani yako ndio silaha yako Mola ndo ajua
Apangalo Mungu mwanadamu hawezi pangua 
Eeh sijali sijali sijali,
Bado napambana
Sijali sijali sijali
Bado napambana

Saa hivi nina mengi mpaka mengine nayasahau
Walileta madharau kweli mi sitosahau
Na si utani dah leo hii kila napopita
Wasiponigusa basi wataniita
Wabaro zao zote zilisita
Wakati wao ndo walioanzisha vita
Na nimewajua wote na nipo nao kivyovote
Walitaka nisote kwenye maisha nisitoke
Na nisifike popote

Imani yako ndio silaha yako Mola ndo ajua
Apangalo Mungu mwanadamu hawezi pangua 
Eeh sijali sijali sijali,
Bado napambana
Sijali sijali sijali
Bado napambana

Kama sio leo kesho kwote ni changamoto
Nitapata wakati wangu upo
Ila mimi sijali yeiyee
Ila mi sijali...

Watch Video

About Sijali

Album : Sijali (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : May 09 , 2021

More ROSE NDAUKA Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl