Nikumbushe Wema Wako by PAUL CLEMENT Lyrics

Nirahisi kinywa kujawa na lawama tele
Pale mambo yanapoonekana hayaendiii
Ni ajabu sana namna moyo unahangaika kutafuta majibu
Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka yakwamba japokuwa Mungu anaishi ndani yangu kuna muda nahofu japokua Mungu anaketi kati yetu kuna muda nahofu
Ahh nakumbuka wana wa Israel katika bahari yashamu japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi
Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwanaa Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa yalibadilika mambo
Manung'unikoo yalisimama na kusahau muujiza alotenda Bwana Mwanzo aah
Eee Mungu Niisaidieee eee eenhee
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee
Nisaidieee kukumbuka baba yakwamba umenichora kiganjani mwako kati ya wengi walioko duniani eenh na mimi umenionaa oooh ooo
Nikumbushe baba yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleniii ouoooh ooh
Yakwamba kama ungeniacha hatua moja nisingelifika nilipo ooh eee Babaa umenikunguta mavumbi kunguta mavumbi mimi na kuniheshimisha
Oooooh oooooh

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu Nisaidie Yesu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozii 

Music Video
About this Song
Album : Nikumbushe Wema wako ,
Release Year : 2016
Copyright : ©2016
Added By: Trendy Sushi
Published: Mar 10 , 2020
More Lyrics By PAUL CLEMENT
Comments ( 0 )
No Comment yet
Leave a comment