Baba Lyrics by NAY WA MITEGO


Thanks God nimeamka salama
Leo nimejikuta tu nakukumbuka baba
Dingi leo nimekuja kwako
Japo sikutokea ata kwenye msiba wako

Stori ni nyingi juu ya kifo chako
Na mama analalamika havimtoshi viatu vyako
Nimeamini kweli kikulacho ki nguoni mwako
Na wale wafuasi wako hawapo upande wako

Ile benki ulojenga kwako sikuizi imekuwa bar
Watu wanakunywa bia na hakuna anayeshangaa
Kile kiwanja cha ndege sijui ungejega tu cha mpira
Hakuna ndege inayotua labda kasuku na njiwa

Uliemwacha mwenezi sio mwenezi tena 
Eti ana shule ya uongozi kifupi wamemtema
Nae kawa kama mpinzani kutwa mama anamsema
Dingi! Huku ni salama ila team yako inatia huruma

Baba baba baba, baba baba baba
Baba baba baba, we baba wee
Baba baba baba, we baba wee
Baba baba baba, babaaa
Baba baba baba, babaaa
Baba baba baba, we baba wee

Dingi najua haukunipenda sababu itikadi zangu
Misimamo yangu na yako, maamuzi yangu
Ndio maana leo kuongea na wewe wanashangaa
Walimwengu hata mama sijui kama ananipenda ka wenzangu

Washikaji wako wa machinga huku hali ni tete
Wanafukuzwa mitaani sijui nani awatetee
Wana mikopo wanasomesha ata sijui wataishije
Na zile 20 zao mlichukua ili iweje

Kipenzi chako saba kala mvua 30 jela
Ila mwanao konda bado yupo uraiani Allah
Na mama anapambana kutulinda na maradhi
Watu wanachanja na anasisitiza twendelee na kazi

Ila wkwa taarifa hii najua haito kushitua
Freeman anasota maabusu anasubiri kuhukumiwa
Dingi mambo ni mengi muda ni mchache
Endelea kupumzika mzee nisikuchoshe

Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulaleeee

Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulale ulale 
Baba baba baba, ulaleeee

Watch Video

About Baba

Album : Baba (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Oct 27 , 2021

More NAY WA MITEGO Lyrics

NAY WA MITEGO
NAY WA MITEGO
NAY WA MITEGO
NAY WA MITEGO

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl