Nitafika Tu Lyrics
Nitafika Tu Lyrics by MAGGIE MULIRI
Nina imani nitafika
Jibu ni kufika
Japo uwoga na wasi wasi
Nitafika niendapo
Jibu kwa moyo mwangu, nitafika eeeh
Natamani kuenda kule nionapo
Nina shauku ya kutekeleza
Maono yangu eeh
Lakini vikwazo ni vingi sana
Lakini majaribu ni mengi sana
Oooh wa kunivunja moyo
Ni wengi sana njiani
Pharao na jeshi lake hawataki kuniacha
Jibu kwa moyo wao, nitafika
Japo milima na mabonde
Nitafika nitafika niendapo oooh
Nahitaji nehema yako Jehovah
Nifike niendapo ooh
Nahitaji msaada wako baba
Nifike niendapo ooh
Naomba nishike mkono
Nifike niendapo
Jibu kwa moyo wangu
Nikufika
Bado nina pumzi, tumaini langu lipo(Nitafika tu)
Sikupata leo, kesho inakuja oooh(Nitafika tu)
Baada ya kesho, mwezi ujao unakuja(Nitafika tu)
Najipa moyo mwaka kesho nitafaulu eeh(Nitafika tu)
Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe(Utafika tu)
Huruma ya Mungu imekutafuta leo(Utafika tu)
Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako(Utafika tu)
Wema wa Mungu umekutafuta leo(Utafika tu)
Nikufika nikufika wee(Utafika tu)
Nikufika nikufika wee(Utafika tu)
Ata usiku uwe mrefu kutakucha
Ata giza iwe kubwa nuru itatokea
Jibu ya maisha yako ipo leo
Ata safari iwe na vikwazo utafika
Hata jaribu liwe nzito utavuka
Jibu ya maisha yako ipo leo
Unamkumbuka Sara alipata mtoto uzeeni
Unamkumbuka Hannah mpaka alichekwa oooh
Kumbe tumboni mwake amembeba Samweli
Nehema ya Mungu bado iko nawe
Yamkini huduma yako imebeba vitu vingi
Hata giza liwe kubwa nuru nayo ipo
Nehema ya Mungu bado iko nawe
Hata maji yawe marefu basi kuna ukingo wake
Nehema ya Mungu bado iko nawe
Huruma ya Mungu bado inakutafuta aah
Nimejitahidi sana bila mafanikio(Nitafika tu)
Haijalishi shida, vikwazo safarini wee(Nitafika tu)
Sijali wangapi wananikatisha tamaa(Nitafika tu)
Wala sitajali mazingira ninayoyapitia(Nitafika tu)
Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe(Utafika tu)
Huruma ya Mungu imekutafuta leo(Utafika tu)
Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako(Utafika tu)
Wema wa Mungu umekutafuta leo(Utafika tu)
Nikufika nikufika wee(Utafika tu)
Nikufika nikufika wee(Utafika tu)
Watch Video
About Nitafika Tu
More MAGGIE MULIRI Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl